Thursday, 5 September 2013

MJANE ANAOMBA MSAADA WA KUTIBIWA MKONO BAADA YA KUJERUHIWA NA NYOKA

Tunomba radhi kwa picha zilizo wekwa kwenye mtandao huuu

Mwanamke Mjane FAINES NAMBEYE KAONGA [60] Mkazi wa kijiji cha IGUNDU Kata ya SANGAMBI Wilaya ya CHUNYA Mkoani MBEYA anawaomba wasamaria kumchangia pesa kwa ajili ya kupata matibabu baada ya kujeruhiwa  na nyoka alipokuwa amelala  chumbani kwake.
Hivi ndivyo mkono wake ulivyo kwa sasa



Mwanamke mmoja Mjane aliyefahamika kwa jina la FAINES NAMBEYE KAONGA [60] Mkazi wa kijiji cha IGUNDU Kata ya SANGAMBI Wilaya ya CHUNYA Mkoani MBEYA anawaomba wasamaria kumchangia pesa kwa ajili ya kupata matibabu baada ya kujeruhiwa  na nyoka alipokuwa amelala  chumbani kwake.

Mjane huyo alijeruhiwa mkono wa kushoto na nyoka alipokuwa amelala chumbani kwake hivi karibuni na kusababisha ngozi kutoka hali iliyomsababishia maumivu makali ambapo alikimbizwa Hospitali ya Wilaya ya CHUNYA na kupatiwa matibabu lakini mpaka sasa hali inazidi kuwa mbaya.

FAINES  amesema pamoja na kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya na kuruhusiwa kurudi nyumbani mkono umezidi kuliwa na sumu na kusababisha ngozi kutoka hadi mfupa kutokeza nje ya ngozi hali inayomtia hofu siku hadi siku.

Mama huyo hana pesa za kuweza kupata matibabu zaidi kutokana nayeye kufiwa na mumewe na wanawe hawana uwezo wa kugharamia matibabu katika Hospitali nyingine hivyo kuwaomba wasamaria wema kumsaidia ili aweze kuokoa maisha.

Baadhi ya majirani wamesema mama huyo ameumwa na nyoka siku za hivi karibuni akiwa amelala chumbani kwake na alipopelekwa kupatiwa matibabu hajapata ahueni na afya yake imezidi kuzorota siku hadi siku hali akishindwa kufanya kufanya shughuli za kiuchumi

Picha na Ezekiel Kamanga
kwa hisani ya Mbeya yetublog

Kwa atakae guswa  kumsaidia mjane huyu wasiliana 
na

0754 49 07 52
AU
0754 37 44 08

0 comments: