Askari
wa usalama barabarani katika wilaya ya Iringa ambae jina lake
halikuweza kufahamika mara moja akiwa amemsimamisha mwendesha
pikipiki aliyepakia abiria (Mishikaki) kinyume na sheria..............................................................................
NA DIANA
BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM
IRINGA
MTU
mmoja amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa baada ya pikipiki walizokuwa
wakiendesha kugongana maeneo ya Ipambasilo kijiji cha Ikuvala kata ya Isele
tarafa ya Mazombe barabara ya Ilula- Uhambingeto wilaya ya Kilolo.
Imedaiwa
marehemu huyo aliyetambulika kwa jina NICOLUS MGATA (15) alikuwa akiendesha
pikipiki aina ya sunlg yenye namba za usajili T.733 BUE aligongana uso kwa uso
na pikipiki aina ya sunlg yenye namba za usajili T.819 CHJ iliyokuwa
ikiendeshwa na JUSTINE CHEWELE (20) mkazi wa ilula.
Akizungumza
na mtandao wa www.matukiodaima.com
kamanda wa polisi mkoa wa Iringa RAMADHANI MUNGI alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo lililotokea tarehe 13 januari mwaka huu.
Hata
hivyo alisema marehemu alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali
ya teule ya itunda huku dereva wa pikipiki bwana CHEWELE amelazwa hospitali ya
mkoa baada ya kuvunjika mguu. Kamanda MUNGI alisema chanzo cha ajali hiyo ni
mwendo kasi.
Wakati
huo huo jeshi la polisi mkoani Iringa linamshimkilia mtuhumiwa mmoja jina
VEDASTO NGODA (28) Mkazi wa masege kwa kosa la kukutwa na kipande cha jino la
tembo pamija na jino la kiboko katika gari lake.
Kamanda
MUNGI alisema tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 14 januari mwaka huu majira ya saa 2:30 usiku maeneo ya
samora kata ya mshindo manispaa ya Iringa ambapo mtuhumiwa huyo alikuwa
akiendesha gari aina ya Toyota mark II lenye namba za usajili T.793 ACP,
alikutwa na vipande hivyo akiwa amevificha chini ya mito ya kukalia.
Aidha
kamanda MUNGI alisema mbali na matukio hayo mawili tofauti, watu wasiofahamika
waliibapikipiki aina ya fecon yenye namba za usajili T.389 CNG mali ya WAZIRI
MSUMBWA(28) ni mfanyabiashara na mkazi wa mwangata manispaa ya Iringa iliyokuwa
ikiendeshwa na SIJALI IDD (25) mkazi wa mlandege.
Dereva
wa pikipiki amekamatwa kwa mahojiano.
0 comments:
Post a Comment