Wednesday, 30 December 2015

SERIKALI YATOA TAMKO ZITO JUU YA BEACH ZOTE ZA TANZANIA , HAYA NDYO MAAGIZOO ......!!!


 













 BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limewataka wawekezaji wa hoteli zilizopo pembezoni mwa bahari kuacha kuwatoza wananchi fedha za kiingilio wanapokwenda katika fukwe hizo kupunga upepo au kuogelea.
Tamko hilo limekuja kutokana na baadhi ya hoteli katika Jiji la Dar es Salaam kubainika kutoza fedha kuanzia Sh 10,000 hadi 40,000 kwa mtu mmoja kama gharama za kuogelea.Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa wamiliki wa hoteli hizo wamekuwa wakifanya hivyo katika sikukuu mbalimbali na zile za mwisho wa mwaka, jambo ambalo limekuwa likileta kero kwa jamii.


Akizungumzia suala hilo Mwanasheria wa NEMC, Manchari Heche, alisema kwa mujibu wa sheria, fukwe zote ni mali ya umma, hivyo wananchi hawatakiwi kutozwa fedha wakati wanapokwenda kutembea au kuogelea.“Kifungu cha 57 cha sheria ya mazingira kimeweka ukomo wa mpaka wa kila kiwanja kilichopo karibu na ufukwe.

“Beach (fukwe) zote ni mali ya umma kwa sababu kuna mipaka yake, hivyo kitendo cha kuwatoza wananchi fedha za kuingia katika fukwe hizo ni kosa kisheria na wanaofanya hivyo wanapaswa kuacha mara moja,”alisema Heche.

0 comments: