Kwa mara ya kwanza katika historia ya Minnesota Timberwolves, iliingia katika NBA Draft ikiwa ya kwanza kuchagua mchezaji wa kwanza kutoka katika vyuo vikuu kwa ujumla.
Timberwolves ilimchagua mchezaji Karl-Anthony Towns ambaye ni mchezaji wa kwanza kutoka katika Jamhuri ya Dominika kuchaguliwa katika nafasi ya kwanza kuingia NBA.
Timu hiyo pia ilishuhudia wachezaji watatu waliochaguliwa katika nafasi ya 1 katika draft tatu mfululizo wakiichezea timu hiyo.Towns alijiunga na Anthony Bennett na Andrew Wiggins kwa wakati mmoja.
Houston Rockets ikawa timu ya kwanza katika historia ya ligi kuanza msimu ikipoteza mechi tatu mfululizo kwa tofauti ya pointi 20 (au zaidi).
Novemba 1, 2015, wachezaji watatu wa San Antonio Spurs (Tim Duncan, Tony Parker na Manu Ginóbili) walifanikiwa kupata ushindi wa 541 wakiwa pamoja. Hii iliwafanya kuwazidi wachezaji Larry Bird, Robert Parish na Kevin McHale wa Boston Celtics kati ya 1981 na 1992. Bahati nzuri ushindi na rekodi ilikuja dhidi ya Boston Celtics.
Novemba 1, 2015, Tim Duncan alifanikiwa kufikisha jumla ya pointi 26000 katika ushindi dhidi ya Celtics.
Novemba 2, 2015, LeBron James alifanikiwa kumzidi Kobe Bryant na kuwa mchezaji mdogo zaidi kuwahi kufikisha pointi 25,000. Alifanya hivyo akiwa na miaka 30, siku 307 katika ushindi dhidi ya Philadelphia 76ers. Pia akawa mchezaji wa 20 katika historia ya ligi kufikia pointi 25,000 siku hiyo.
Novemba 2, 2015, Tim Duncan alipata ushindi wake wa 954 akiwa na San Antonio Spurs katika ushindi wa 94-84 dhidi New York Knicks katika uwanja wa Madison Square Garden, na hivyo kuwa mchezaji aliyeshinda michezo mingi zaidi akiwa na timu moja.
Novemba 7, 2015, Tim Duncan alicheza katika mechi yake ya 1336 katika maisha yake ya NBA, alipanda mpaka katika nafasi ya 10 kwenye orodha ya muda woteya wachezaji waliocheza michezo mingi akimpita mchezaji Gary Payton.
Novemba 11, 2015, Tim Duncan alipanda mpaka katika nafasi ya 7 katika orodha ya muda wote ya wachezaji waliodaka rebound nyingi, akimpita mchezaji wa zamani wa Boston Celtics Robert Parish.
Novemba 14, 2015, Tim Duncan alipanda mpaka katika nafasi ya 5 kwenye orodha ya wachezaji wenye blocks nyingi. Alimpita mchezaji mwenzake wa zamani na Hall of Famer David Robinson. Bahati nzuri mchezaji mwenzake Tony Parker pia akawa mchezaji wa 34 kutoa pasi/assist 6,000.
Novemba 15, 2015, Kevin Garnett akawa mchezaji wa tano katika historia ya ligi ya kucheza zaidi ya dakika 50,000, ikiwa ni pamoja na kumzidi Elvin Hayes katika nafasi ya nne kama mchezaji aliyetumika zaidi. Aliweza kufikia rekodi hiyo baada ya kucheza dakika 23 katika mchezo waliopoteza dhidi ya Memphis Grizzlies.
Novemba 17, 2015, LeBron James alimzidi Jerry West katika kipindi cha robo ya kwanza ya mchezo waliopoteza kwa Detroit Pistons katika nafasi ya 19 ya ufungaji wa muda wote.
0 comments:
Post a Comment