Thursday, 31 December 2015

Zaidi ya milioni 389 za miradi ya wananchi wilayani Mvomero zimetumika bila mpangilio.


Kiasi cha shilingi zaidi ya milioni 389 zilizotolewa na serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika kijiji cha Bunduki tarafa ya Mgeta wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro zimepotea bila kufanya kazi zilizokusudiwa zikiwemo fedha za mradi mkubwa wa maji safi,mradi wa umwagiliaji pamoja na  ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari Bunduki.

Akifafanua ubadhilifu wa fedha uliofanyika wakati wa utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji uliogarimu zaidi ya milioni 251 mwenyekiti wa kijiji cha Bunduki Michael Segelo amesema kijiji chake hakikushirikishwa katika utekelezaji na baada ya mradi kukamilika mwezi Novemba mwaka huu hawakukabidhiwa na haujawahi kutoa maji. 
 
Kwa upande wake diwani wa kata ya Bunduki Bwana Prosper Mkunule amesema hatakubali kuona fedha za wananchi zinapotea bure na kwamba afuatilia hadi waliohusika na ubadhilifu huo watakapochukuliwa hatua. 
 
ITV imemtafuta aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mvomero wakati miradi hiyo inafanyika ili kuzungumzia sakata hilo  Bwana Wallas Karia ambaye amesema yeye alisha hamia manispaa ya Bukoba huku jitihada za kumtafuta mhandisi wa maji wa wilaya ya Mvomero Bwana Gabriel Ngongi zikigonga mwamba baada ya simu yake kutopatikana na kwa wakati huo. 

0 comments: