Thursday, 31 December 2015

Shirika la umeme nchini Tanesco limefanikiwa kuwanasa watu wanaoiba umeme Rukwa

 
Shirika la ugavi wa umeme Tanesco mkoani Rukwa,limefanikiwa kuwabaini zaidi ya wateja kumi na mbili wa shirika hilo wasiokuwa waaminifu, kufuatia msako mkali unaoendelea hivi sasa,wanaotumia umeme bila ya kuulipia kama inavyompasa kila mteja,kwa kujiunganishia umeme kwa njia za ujanja ujanja na kuzifanya mita zao zisishindwe kusoma umeme unaotumika kwa usahihi.

Afisa mahusiano wa shirika hilo la umeme la Tanesco kwa mkoa wa Rukwa Bw.Samweli Mandari,akiongea kwenye maeneo ya kizwite mjini Sumbawanga wakati zoezi la kuwasaka wateja wasiokuwa waaminifu, amesema baadhi ya mafundi umeme wasiokuwa waaminifu wamekuwa wakila njama na wateja wa umeme,ili waweze kutumia umeme bila ya kulipia malipo sahihi,jambo ambalo linaliingizia shirika hilo hasara kubwa na wala halifai kufumbiwa macho.
 
Mmoja wa watuhumiwa ambaye ni mpangaji wa nyumba iliyokutwa na matatizo ya kujiunganishia umeme kwa njia isiyokuwa halali, katika mtaa wa mtumbuka maeneo ya Kizwite manispaa ya Sumbawanga Bi Elizabeth Pangipita, amejitetea kuwa yeye alikuwa hajui lolote linaloendelea kwa vile pamoja na mpangaji mwenziwe walikuwa wakichangia malipo ya umeme,na kumpatia mwenye nyumba aliyesema kuwa yupo safarini.

0 comments: