>>> Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameanza ziara mkoani Kigoma huku akiahidi kuanza ujenzi wa reli mpya ya kisasa ya viwango vya ‘standard gauge’, itakayosaidia kuimarisha biashara ya kusafirisha mizigo kutoka Dar es Salaam kwenda nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), kupitia Bandari ya Kigoma.
Tamko la Waziri Mkuu Majaliwa inaashiria kuanza kwa utekelezaji wa vipaumbele 25, ikiwamo ujenzi wa reli ya kati, alivyovitoa Rais John Magufuli (wakati huo akiwa mgombea urais wa CCM), Agosti 24, wakati wa uzinduzi wa kampeni zake kwenye Viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam
0 comments:
Post a Comment