Unakumbuka au umwahi kusikia zile headlines za mtu mnene kuliko wote duniani, basi imenifikia stori yake mpya japokuwa sio njema mtu wangu. Andres Moreno jamaa ambaye anashikilia rekodi ya kuwa mtu mnene duniani amefariki dunia December 25 siku ya sikukuu ya Chrismas.
Stori kutoka indianexpress.com zinaeleza Andres Moreno ambaye alikuwa anatajwa kuwa na uzito wa Kilogram 450 ameaga dunia asubuhi ya December 25 siku ya Chrismass kwa tatizo la moyo, tatizo ambalo limetokana na kuwa mnene kupita kiasi. Andres Moreno amefariki akiwa na umri wa miaka 38.
Licha ya jitihada za kuokoa maisha yake kufanyika kwa kuchukuliwa na Ambulace kutoka nyumbani kwake Sonora Mexico na kuwahishwa St Jose Hospital, lakini jitihada hizo hazikuzaa matunda. Ripoti ya madaktari imetoka jana December 26 kuhusu tatizo lililopelekea kuchukua uhai wake.
0 comments:
Post a Comment