Wednesday, 30 December 2015

HAMISI ANDREA KIGWANGLA AKIZA KITUO CHA CHA AFYA CHA KAMBARAGE WATUMISHI NDANI YA MIEZI 3

 
--> Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla ameuagiza uongozi wa Kituo cha Afya cha Kambarage mjini Shinyanga kuhakikisha unapata watumishi wa kutosha ndani ya kipindi cha miezi mitatu.

Dk Kigwangalla alitoa maagizo hayo baada ya kutembelea kituo hicho na kusikiliza uongozi wa kituo na malalamiko ya wagonjwa wanaofika kupata huduma.
Naibu waziri huyo, ambaye wizara yake inahusika pia na masuala ya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, aliutaka uongozi huo kufanya tathmini ya upungufu wa watumishi.

Mbali na kutoa maagizo hayo, Dk Kigwangalla aliwataka wafanyakazi wa kituo hicho kuhakikisha wanafanya kazi ya kuwahudumia wagonjwa badala ya kuwahi kazini na kujifungia ofisini

0 comments: