Monday, 28 December 2015

WHO kutangaza Guinea nchi isiyo na Ebola

Image copyright 
Image captionMgonjwa wa mwisho wa Ebola Guinea
Shirika la Afya Duniani leo inatarajiwa kuitangaza Guinea kuwa nchi isiyo na maambukizo ya ugonjwa wa Ebola.
Mlipuko wa virusi vya ugonjwa wa Ebola ulianza nchini humo miaka miwili iliyopita.
Ugonjwa wa Ebola umesababisha vifo vya maelfu ya watu katika nchi za Afrika magharibi, hususan katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone.
Waguinea wanajiandaa kusherehekea kumalizika kwa janga hilo nchini mwao kwa kufanya maonesho na kurusha fataki.
Wengi wanasema wanaanza mwanzo mpya na mwaka mpya na pia kwa rais wao Alpha Conde ambaye muhula wake wa uongozi ulianza wiki iliyopita.
Hata hivyo ugonjwa wa Ebola umeweka kumbukumbu mbaya nchini humo, hususan athari za kijamii na kiuchumi.
Kwa mujibu wa Shirika la Kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, nchini humo watoto 6,220 wameachwa yatima kwa kupoteza mzazi mmoja ama wote wawili kutokana na ugonjwa huo.
Wale walioathiriwa na ugonjwa huo, pia bado wanaishi kwa hali ya mashaka na kubaguliuwa.

0 comments: