-
-> Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) haiwezi kukaa kimya huku ikishuhudia raia wa Burundi wakifa bila ya kuwa na hatia.
Akizungumza kwenye mkutano wa amani jana uliofanyika Entebbe nchini Uganda, Museveni alisema mauaji ya raia yanayoendelea Burundi yanatishia usalama wa nchi hiyo na kuhatarisha kutokea kwa mauaji ya kimbari.
“ Sikutaka kuwa miongoni mwa wapatinishi kwa sababu nilifanya hivi nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), tukakubaliana kabisa kuhusu amani, lakini nikaonekana sijafanya kitu kwani baada ya kumalizika kwa mkutano ule machafuko yakaendelea,’’ alisema Museveni na kuongeza kuwa: ‘’Lakini Mungu amenipa afya kwa nini nisiwasaidie watu wa Burund, nataka kuona makubaliano haya yanafikiwa mwafaka kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Uganda.’’
0 comments:
Post a Comment