- Lionel Messi ametangwazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka kwenye tuzo za Globe Soccer
- Barcelona imeshinda tuzo ya klabu bora ya mwaka
- Tuzo ya Player career imekwenda kwa Andrea Pirlo na Frank Lampard
- Jorge Mendes amepewa tuzo ya wakala bora wa mwaka
Super Star wa klabu ya Barcelona Lionel Messi amenyakua tuzo ya mchezaji bora wa mwaka ya heshima iliyotolewa na Globe Soccer, Dubai.
Mabingwa wa La Liga Barcelona ambao walitwaa mataji matatu (treble) msimu uliopita walitangazwa kama klabu bora ya mwaka wakati Josep Maria Bartomeu (Rais wa klabu ya Barcelona) alitangazwa kama rais bora wa klabu wa mwaka.
Mshambuliaji huyo wa Argentina, alifanikiwa kupachika mabao 58 na kuisaidia Barcelona kunyanyua ndoo tatu msimu uliopita.
Wakongwe wanaokipiga kwenye klabu ya New York City Andrea Pirlo na Frank Lampard wao walitwaa tuzo ya heshima kutokana na mchango wao katika soka (Player Career Award).
Jorge Mendes ambaye pia ni wakala wa super star wa Real Madrid Cristiano Ronaldo yeye alitwaa tuzo ya wakala bora wa mwaka, kocha wa Ubelgiji yeye akatangazwa kama kocha bora wa mwaka.
Wakati huohuo klabu ya Benfica ilitwaa tuzo ya Best Academy of the Year, Ravshan Irmatov alitajwa kama mwamuzi bora wa mwaka .
0 comments:
Post a Comment