Tuesday, 29 December 2015

SIMBA YAWACHOKA WAAMUZI KUTOKA MBEYA, MWANZA, SHINYANGA, YAANDIKA BARUA WASIICHEZESHE KABISA

RAIS WA SIMBA, EVANS AVEVA (ANAYEZUNGUMZA) KULIA KWAKE NI MAKAMU WAKE, GEOFREY NYANGE 'KABURU' NA MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI YA SIMBA, JASMINI B. COSTA.

Uongozi wa juu wa Simba umeandika barua kwa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) kupinga kuchezeshwa tena na waamuzi wanne.

Simba imewakataa waamuzi walioichezesha katika mechi dhidi ya Mwadui FC ambayo iliisha kwa wao kutoka sare ya bao 1-1.

Rais wa Simba, Evans Aveva amewaambia waandishi leo kwamba wameamua kufanya hivyo baada ya kuona wazi waamuzi wale waliamua 'kuimaliza' Simba kwa makusudi kabisa.

Sare hiyo, Simba walilazimika kusawazisha ‘jioni’ kupitia Brian Majegwa ambaye aliingia kipindi cha pili.

Waamuzi ambao Simba imewakataa kwa madai waliiminya kwa makusudi kabisa ni Ngole Mwangole-Mbeya, Joserph Masija-Mwanza, Silvestre Mwanga-Kilimanjaro na Mdogo Makame-Shinyanga.

0 comments: