Tuesday, 29 December 2015

MCHEZAJI AFUKUZWA BARCELONA MASAA TU BAADA YA KUSAINI mkataba

 

BARCA-Sergi-Guardiola-AFUKUZWAMASAA machache tu baada ya kusainiwa kuichezea Timu ya Rizevu ya Barcelona huko Spain, Fowadi Sergi Guardiola alifukuzwa kutoka Timu hiyo.
Guardiola, mwenye Miaka 24, alijiunga na Barcelona B Jana Jumatatu na Masaa machache baadae Maofisa wa Barca wakapewa tipu kuwa Mchezaji huyo alitoa posti kwenye Mtandao wa Twitter akiiponda Barcelona na Jimbo la Catalonia ambalo Barca wanaliunga mkono na ambalo linataka kujitenga toka Spain huku pia akiisapoti Real Madrid ambao ni Mahasimu wa Barca.
Guardiola alisajiliwa kutoka Klabu ya Jijini Madrid,, Alcorcon, inayocheza Ligi Daraja la Pili huko Spain, Segunda B.
LA LIGA
Ratiba
**Saa za Bongo
Jumatano Desemba 30
1800 Real Madrid CF v Real Sociedad
1800 Levante v Malaga CF
2015 Rayo Vallecano v Atletico de Madrid
2015 Sevilla FC v RCD Espanyol
2030 SD Eibar v Sporting Gijon
2230 FC Barcelona v Real Betis
2230 Celta de Vigo v Athletic de Bilbao
2230 Getafe CF v Deportivo La Coruna
2300 Las Palmas v   Granada CF
Alhamisi Desemba 31
1800 Villarreal CF v Valencia C.F

0 comments: