Tuesday, 29 December 2015

msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara 2015/16 hii hapa

 

Jumapili Desemba 27
Azam FC 2 Kagera Sugar 0
Toto Africans 0 African Sports 1
+++++++++++++++++++
LIGI KUU VODACOM, VPL, iliendelea Leo kwa Mechi 2 ambapo huko Azam Complex, Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam, Azam FC waliichapa Kagera Sugar 2-0 na huko CCM Kirumba Jijini Mwanza Wenyeji Toto Africans walitunguliwa 1-0 na African Sports.
Huko Chamazi, Azam FC walifunga Bao lao la kwanza Dakika ya 9 kupitia Kipre Tchetche VPL-DES27aliefunga kwa Kichwa akiunganisha Kona ya Himid Mao.
Kagera Sugar walikosa nafasi safi ya kusawazisha katika Dakika ya 35 walipopewa Penati lakini Mkwaju wa Salum Kanoni ulichezwa na Kipa Aishi Manula.
Bao la Pili la Azam FC lilifungwa na Shomari Kapombe katika Dakika ya 74 na kuwapa ushindi wa 2-0 ambao sasa umewafanya wawakaribie Vinara Yanga wao wakiwa Nafasi ya Pili Pointi 1 nyuma yao huku wakiwa na Mechi 1 mkononi.
Sasa Azam FC wana nafasi murua kuipiku Yanga kwenye Mechi yao ya kiporo watakayocheza na Mtibwa Sugar hapo Jumatano Desemba 30 ikiwa watashinda.

LIGI KUU VODACOM
Desemba 26
Matokeo:
Yanga 3 Mbeya City 0
Coastal 1 Stand United 3
Mtibwa Sugar 3 JKT Mgambo 0
Mwadui FC 1 Simba 1
Ndanda FC 1 JKT Ruvu 3
Majimaji FC 0 Tanzania Prisons 2

0 comments: