Baada ya miaka 6 ya kuugua Ariel Sharon Waziri mkuu wa Israel Afa,Mataifa ya Kiaraba watoa salamu za rambirambi.
Kwa mujibu wa kitengo cha upasuaji wa
Hospitali alikolazwa ambako iko katika Ardhi inayokaliwa kwa mabavu na
Taifa hilo la Kizayuni katika mji wa Bi'ro Sab'a waziri mkuu wa zamani
Ariel Sharon ambae atakumbukwa kwa kumwaga damu za waislaam wa
Falastine,Sharon alikata roho tarehe 02.08.013 saa 17:31.
Madaktari waliokuwa wakimhudumia Ariel Sharon ambae kwa miaka sita alikuwa katika hali isiyoeleweka ya kutokuwepo duniani wala akhera,na jana kwa mara ya kwanza kabisa alikata roho.
Madaktari waliokuwa wakimhuduhumia wakati akiugua Mal'uni huyo wamesema "Sisi kama ni juhudi kwa kadri ya uwezo wetu tumefanya,lakini tunasikitika Ariel Sharon amekufa amekwenda Waziri mkuu wa Zamani wa Israel" .
Televisheni ya Israel ya 12 imetangaza kuwa mataifa ya nchi za kiarabu wametuma salaam za Rambi Rambi kwa Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netenyahu kutokana na kuondokewa na mtu muhimu kwa Taifa la Kizayuni ya Isreal,Vyombo vya habari vya Israel imewapongeza kwa utawala wa Falme za Dubai kwa kuguswa na kifo cha Ariel Sharon.
Ariel Sharon ameadhibiwa hapa hapa Duniani na amepitia marhala mbalimbali alipokuwa kiugua na kupata maumivu makali kabla hajapelekwa Akhera,alinyonya Damu za wanawake na watoto wa Falastine na wanajeshi wake amewaingiza vitani
Kuna baadhi ya vyanzo vya habari viliyokuwa vikieleza kuwa Ariel Sharon alikufa muda mrefu lakini utawala huo wa Kiyahudi ulificha kutokana na khofu ya kushambuliwa kwa wanajeshi wake na mataifa ya kiarabu iliyoingia katika vugu vugu la mabadiko la kisiasa.
0 comments:
Post a Comment