Tuesday, 14 January 2014

MAULID YA KUZALIWA BWANA MTUME (S.A.W) ILIYOFANYIKA HUKO ZANZIBAR

 Baadhi ya Viongozi wa Srikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na mashekhe waliohuduria katika Maulidi ya kuzaliwa Bwana Mtume (S.A.W.) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Unguja.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
TA1A1152 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Sheikh Sherali Champsi Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maulidi ya kuzaliwa Bwana Mtume (S.A.W.) alipowasili katika viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Unguja  palipofanyika Maulid hayo jana.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
TA1A1162 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi wengine (kutoka kushoto) Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Mohamed Gharib Bilali,Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, na (kulia) makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamadi,wakiwa katika Maulidi ya kuzaliwa Bwana Mtume (S.A.W.) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Unguja.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
TA1A1163 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiteta jambo na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi  katika Maulidi ya kuzaliwa Bwana Mtume (S.A.W.) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Unguja.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] TA1A1166 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi wengine wakisimama kumswalia Mtume (S.A.W.) wakati wa Maulidi ya Kusherehekea siku ya Kuzaliwa Bwana Mtume katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Unguja jana.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
TA1A1171 
Wake wa Viongozi na wanawake kutoka madarasa na vyuo mbali wakiongozwa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein wakiwa katika Viwanja vya Mnazi mmoja Mjini Unguja katika Maulid ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtuyme (S.A.W.).[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
 
TA1A1218 
Wake wa Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakisimama kumswalia Mtume (S.A.W.) wakati wa Maulidi ya Kusherehekea siku ya Kuzaliwa kwake  Mtume katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Unguja jana.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Related Posts:

0 comments: