Akiongea na wadau wa mfuko huo 
mapema leo Jijini Arusha, , Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Crinsetus 
Magori, alisema kuwa mpaka sasa tayari mfuko huo ulishaanza kufanya 
mazungumzo ba wadau mbalimbali wa michezo hapa nchini ili kuweza kuokoa 
maisha ya wachezaji
Magori alidai kuwa mpango huo 
utaanza rasmi mwakani na utaweza kuwanufaisha wachezaji mbalimbali hasa 
wale ambao wanachezea ligi kuu kama zilivyopangwa.
“tunataka kuona kuwa wachezaji 
wetu nao wanakuwa na mafao nah ii itaweza kuwajengea tabia ya 
kujiwekezea akiba kwa ajili ya maisha yao ya hapo baadae lakini kama 
wakiwa na mafao pia itasaidia kupata mahitaji ya muhimu hasa pale 
wanapokabiliwa na majanga kama ugonjwa pindi wanapokuwa 
uwanjani”aliongeza Magori
Magori alisema ni jambo la 
kusikitisha kuona au kusikia mchezaji akiumwa anakosa fedha ya kujitibia
 wakati kama angekuwa amejiunga na
NSSF, angepata matibabu katika hospitali aliyeichagua bila malipo yoyote.
Magori, alisema kuwa NSSF, 
imeamua kuboresha huduma zake kwa kupanua wigo wa uandikishaji wanachama
 ikiwemo wachezaji wa ligi kuu ambao fedha zao zitakuwa zikikatwa moja 
kwa moja kutoka kwa wafadhili wa ligi hiyo.
“NSSF tumedhamiria kuboresha 
huduma zetu na kujitanua zaidi, wachezaji ni miongoni mwa walengwa wakuu
 baada ya kukamilisha kuwaandikisha wakulima na wachimbaji 
madini…tarajieni makubwa zaidi” alisema
Awali Mbunge wa Kigoma Kaskazini 
Zitto Kabwe alisema kuwa wachezaji hapa pamoja na wana sanaa mbalimbali 
katika Nchi ya Tanzania wanakuwa maarufu pindi wanapochezea timu 
mbalimbali lakini wanapoacha kucheza kutokana na sababu mbalimbali 
wanajikuta wakiwa wanaishi kwenye maisha magumu tofauti na majina yao 
kwenye jamii.
“Leo nimezungumza na Katibu Mkuu 
wa Simba, kaniambia kuanzia mwakani wachezaji wa timu hiyo wataingia 
katika mfumo wa kukatwa fedha zao na kuzipeleka NSSF ili wapate mafao 
saba yanayotolewa na mfuko huo, ningependa NSSF muangalie kundi hilo.
 






 
 
 
 






0 comments:
Post a Comment