IMEWEKWA SEPTEMBA 6, 2013 SAA 6:37 USIKU
TULIJUA
England wako hatarini kufuzu kushiriki kwenye Kombe la Dunia, tulijua
timu ya vijana chini ya miaka 21 ya England haitavuka hatua ya Makundi
katika michuano ya Ulaya wakati wa kiangazi – walifungwa mechi zote tatu
wao wakifunga bao moja tu.
Tulijua
timu ya vijana ya England chini ya miaka 20 itafanya vibaya wakati wa
michuano ya dunia Uturuki na kabla ya kutoka katika hatua ya makundi.
Timu ya England chini ya miaka 20 haijawahi kushinda mechi tangu wakati
Jamie Carragher na Michael Owen walipoichezea mwaka 1997.
Kaa pembeni Waingereza: Brendan Rodgers hajasajili hata mchezaji mmoja wa nyumbani wakati wa kiangazi
Tunacheki pembeni: Manuel Pellegrini na Arsene Wenger wameamua kuamini vipaji vya nje.
Klabu ambazo hazijanunua Waingereza
Arsenal (wametumia pauni mil 42.5 kwa wachezaji wanne)
Chelsea (wametumia pauni mil 65.5 kwa wachezaji nane)
Liverpool (wametumia pauni mil 23.3 kwa wachezaji nane)
Manchester City (wametumia pauni mil 94.9 kwa wachezaji watano)
Manchester United (wametumia pauni mil 28.5 kwa wachezaji wawili)
Newcastle (Hajatumia kitu, wachezaji wawili, japokuwa mkopo wa Loic Remy ni pauni milioni 2)
Southampton (wametumia pauni mil 35.5 kwa wachezaji watatu)
Stoke (wametumia pauni mil 7 kwa wachezaji sita)
Tottenham (wametumia pauni mil 97.5 kwa wachezaji saba)
NB: Everton na West Brom wamesajili wachezaji wawili tu wa England kwa mkopo (Gareth Barry na Scott Sinclair)
Lakini
usajili wa majanga kwenye soka la England unazidi kuwa kwenye hali
mbaya, BIN ZUBEIRY inaangalia jinsi ambavyo klabu za Ligi Kuu England
zinawapotezea wachezaji wazawa.
Klabu
zimefanya usajili wa jumla ya wachezaji 150 wakati huu wa kiangazi, ni
34 tu (asilimia 22.66) kati ya 150 ndiyo Waingereza.
Chakusikitisha
zaidi klabu sita kati ya saba ambazo zimemaliza kwenye saba bora msimu
uliopita - Manchester United, Manchester City, Chelsea, Arsenal,
Tottenham, Liverpool – zote hazijasajili mchezaji hata mmoja wa
Kiingereza.
Everton,
ambayo ilimaliza nafasi ya sita imesajili mchezaji mmoja wa England,
Gareth Barry tena kwa mkopo – hii inaonyesha ni jinsi gani vipaji vya
wazawa vinakazi kutoka.
Kwa
upande wa Fulham, ambao huwa wanachukua wachezaji wa mataifa mbalimbali
wamenunua wachezaji wawili wa England - Darren Bent (29) ambaye
alishindwa kuvuma Aston Villa na Scott Parker (32) umri umemtupa mkono.
Mbelgiji: Marouane Fellaini alikuwa usajili mkubwa wa David Moyes kwenye dirisha hili la usajili.
Pauni mil 15.5: staa wa West Ham, Andy Carroll alikuwa mchezaji wa Kiingereza mwenye thamani kubwa zaidi wakati huu wa kiangazi.
Wamenunuliwa: Steven Caulker na Jonjo Shelvey walihnunuliwa kwa pauni mil 9 na pauni mil 6
Wachezaji wa England walionunuliwa wakati wa kiangazi
Aston Villa - Jed Steer
Cardiff - Steven Caulker, Simon Moore, John Brayford
Crystal Palace - Dwight Gayle, Jack Hunt, Jerome Thomas, Kevin Phillips, Jason Puncheon (mkopo), Neil Alexander, Steven Dobbie, Barry Bannan
Everton - James McCarthy, Gareth Barry (mkopo)
Fulham - Scott Parker, Darren Bent (mkopo)
Hull - Tom Huddlestone, Curtis Davies, Steve Harper, Danny Graham (mkopo), Jake Livermore (mkopo), George Boyd, Allan McGregor
Norwich - Nathan Redmond, Carlo Nash, Gary Hooper
Sunderland - Duncan Watmore
Swansea - Jonjo Shelvey, Jernade Meade
West Brom - Scott Sinclair (mkopo), Lee Camp
West Ham - Andy Carroll, Danny Whitehead
Katika
ya klabu zilizosajili waingereza ni Swansea, Sunderland, Aston Villa na
West Brom wachezaji hawako kwenye akili za makocha.
Michael Laudrup amesajili wachezaji 10 wawili tu kati yao ni waingereza Jonjo Shelvey na Jernade Meade, kinda kutoka Arsenal.
Paul
Lambert, msimu uliopita alisifika sana kwa kuwapa nafasi Waingereza
kama Matt Lowton na Ashley Westwood, lakini safari hii ameenda kusajili
wachezaji sita kutoka nje na mmoja tu wa England Jed Steer kipa wa
vijana chini ya miaka 19 kutoka Norwich.
Paulo
Di Canio amesajili wachezaji 14 – mmoja tu Muingereza ambaye anamiaka
19 Duncan Watmore kutoka klabu isiyokuwa na ligi ya Altrincham.
Asilimia 50 ya wachezaji wa wazawa waliosajiliwa wakati huu wa kiangazi wamesajiliwa na timu zilizopanda daraja.
Na
wachezaji hao ni wale ambao wanahaha kufufua vipaji vyao. Tom
Huddlestone na Jake Livermore pale Hull, wanahaha kurudisha vipaji vyao
baada ya kuuzwa na Spurs, na hawapo hata kwenye akili ya Roy Hodgson
wakati Danny Graham alichemka Sunderland na sasa anajaribu bahati yake
kwenye uwanja wa KC.
Kutoka Urusi: Willian ameigharimu Chelsea pauni mil 32 kutoka Anzhi Makhachkala
Muhimu: Wabrazil Paulinho na Fernandinho ni mfano kwa klabu kubwa kutoka
Umri tatizo England
35 - Frank Lampard
33 - Steven Gerrard
32 - Ashley Cole, Michael Carrick
31 - Phil Jagielka, Rickie Lambert
30 - Jermain Defoe
29 - Glen Johnson
28 - Leighton Baines, Ashley Young
27 - Wayne Rooney, Gary Cahill, James Milner
26 - Joe Hart, John Ruddy
25 - Fraser Forster
24 - Theo Walcott, Tom Cleverley
23 - Chris Smalling, Kyle Walker, Daniel Sturridge
22 - Andros Townsend, Danny Welbeck
21 - Phil Jones, Jack Wilshere, Steven Caulker
19 - Ross Barkley
18 - Raheem Sterling
Kevin
Phillips, Jerome Thomas na Jason Puncheon wametua Crystal Palace ni
bora zaid kwa klabu hiyo. Simon Moore kipa namba mbili wa Cardiff,
ametoka klabu ya daraja la kwanza ya Brentford.
Idadi inathibitisha tatizo linalohatarisha fursa za wachezaji wa England wa kizazi cha sasa na kijacho.
Mwenyekiti
mpya wa FA, Greg Dyke, amechukua nafasi ya David Bernstein na ni rahisi
kwa wachambuzi kuandika kutaka kuona mabadiliko. Timu ya taifa ya
England inasimamiwa na FA na chama hicho kinatakiwa kulinda mustakabali
wa wachezaji wa England.
Sheria
yoyote itakayotungwa inaweza kuingiliwa na sheria za soka za Ulaya,
mfano wakiamua kuweka sheria ya kutumia wachezaji sita wa England katika
kila mechi sheria za Ulaya zitatengua hilo.
Ukweli
ambao ni mgumu kuukubali ni kwamba Ligi Kuu England ni ligi ya dunia na
FA imeshazidiwa nguvu. Tangu ilipojitenga mwaka 1992 na kuzubaa kwa FA
imeruhusu ligi hiyo kuwa juu zaidi kwenye soka la England.
Babu: Frank Lampard ndiyo anaumri mkubwa zaidi kwenye kikosi cha sasa cha England miaka 35.
Kadiri
mikataba minono ya matangazo inavyozidi kuingiwa ni pigo kwa Ligi Kuu
na Klabu zake. Timu zinakuwa zikihaha kufanya biashara zaidi na FA
inabaki ikiangalia nidhamu tu.
Maendeleo
ya wachezaji wa England yako mikononi kwa klabu za ligi kuu. Lakini
sasa hivi hawaaminiki tena, klabu zimezidi kujuza watoto kutoka nje ya
England kwenye timu zao za vijana.
Sura mpya: Ross Barkley (19) na Raheem Sterling (18) ndio wachezaji makinda zaidi kwenye kikosi cha England.
Na
wakati huu ligi inaingia kwenye msimu mpya timu ya taifa sasa mashabiki
wa England wanaachwa wakiwa na hofu juu ya mustakabali wa muundo wa
timu yao ya taifa siku zijazo.
Hatari
zaidi iko kwa Wales ambao safari hii hakuna hata mchezaji mmoja
aliyesajili wa timu za ligi kuu, lakini Gareth Bale anawabeba kwa kwenda
Hispania.
habari Kwa msaada wa binzubery blog
0 comments:
Post a Comment