NA BASHIR NKOROMO, TABORA
Chama
Cha Mapinduzi (CCM) leo kinatarajiwa kuuteka mji wa Tabora, wakati
Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana atakapohitimisha ziara yake ya siku
kumi mkoani Tabora kwa kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara kwenye
Uwanja wa shule ya Sekondari Uyui.
Kulingana
na ratiba iliyopo, kabla ya mkutano huo mkubwa utanaotarajiwa
kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi kutokana na kuonekana kupaniwa na
wananchi wengi mjini hapa, Kinana atafanya shughuli mbalimbali za
ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya CCM kwa kutembelea miradi kadhaa ya
maendeleo na kuzungumza na wananchi ili kusikiliza kero zao na
kujadiliana nao njia ya kuzitatua.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye ameambatana na Kinana katika
ziara hiyo amesema, Kinana anatarajiwa kuwasili leo asubuhi mjini Tabora
akitokea wilaya mpya ya Kaliua ambako jana alikuwa katika mawendelezo
wa ziara hiyo.
Amesema
mapokezi ya Kinana na msafara wake kutoka kaliua yatafanyika eneo la
Azimio saa nne asubuhi, na baadaye kwenda Kata ya Tumbi kuweka jiwe la
msingi Ofisi ya CCM ya kata hiyo kabla ya kuendelea na safari yake
kuingia Tabora mjini.
Maeneo mengine ambayo Kinana atachapa kazi leo mjini Tabora yametajwa kuwa ni Kinaia, Hospitali ya Kitete, Tambukareli, Gongoni, Soko Kuu la Tabora na Kanyenye.
Hadi kukamilisha ziara yake Kinana atakuwa ametembelea wilaya zote sita za mkoa wa Tabora, akiwa amesafiri zaidi ya kilometa 2,000. Wilaya hizo ni, Igunga, Nzega, Uyui, Sikonge, Urambo, Kaliua na wilaya ya Tabora.
0 comments:
Post a Comment