Msanii
maarufu wa filamu za maigizo
hapa nchini, Adam Kuambiana amefariki Jana mida ya saa 5 asubuhi, huku
kifo chake kikiambanata na hofu ya ugonjwa wa homa ya dengu unaotikisa
nchi kwa sasa.
Kuambiana aliyekuwa akifahamika kwa
kuwa mmoja wa wasanii wenye msimamo, alifariki dunia wakati akipelekwa Zahanati
ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar.
Kabla alikutwa ameanguka chooni
kwenye chumba alichopanga katika nyumba ya wageni ya Silver Rodge iliyopo Sinza
Kwa Remmy jijini Dar.
Mhasibu wa Silver Rodge ambaye alikataa kutaja jina lake
alisema baada ya kumkimbiza msanii kwenye zahanati hiyo daktari alimpima na
kuwaambia kuwa msanii huyo ameshaaga dunia.
Mwili wa msanii huyo umepelekwa
kwenye chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya muhimbili.
MAREHEMU KUAMBIANA WAKATI WA UHAI WAKE (KATIKATI) HII NI FILAMU YA LOST SON, MOJA YA ZILE ALIZOIGIZA NA KUONYESHA UWEZO WAKE. |
Hata hivyo, kumekuwa na hofu ya
ugonjwa huo wa homa ya dengue kwa kuwa moja ya viungo vyake wazi vya mwili,
vilikutwa vimetokwa na damu nyingi sana.
Huenda majibu ya mwisho ua uchunguzi
wa mwili wake, yatatoa majibu sahihi kuhusiana na kifo cha msanii huyo.
KWA MASIKITIKO MAKUBWA, NAWAPA POLE FAMILIA YA MAREHEMU PAMOJA NA WASANII WA FILAMU NCHINI.
MWENYEZI MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA.
0 comments:
Post a Comment