Wanajeshi wa Urusi katika jimbo la Crimea, Kusini mwa Ukraine.
Rais Vladimir Putin wa Urusi amewaamuru wanajeshi wake waliohusika katika luteka za kijeshi ambazo baadhi zikifanyika karibu na Ukraine warudi kwenye kambi zao. Hayo ni kwa mujibu wa msemaji wake Dmitri Peskov.
Luteka hizo zilizokuwa na lengo la kuonyesha utayarifu wa majeshi ya Urusi, ni jambo lililozitia wasiwasi serikali za nchi za magharibi baada ya Urusi kutuma mamiaya wanajeshi katika eneo lina Ukraine la Crimea am
bako wakaazi wake wengi ni wenye asili
ya urusi, ikiwa ni baada sya kuangushwa rais wa zamani Viktor
yanukovich na wapinzani wanaoelemea upande wa magharibi.
"Luteka hizo zilizoanza wiki iliopita zitamalizika kama ilivyo pangwa,"hivyo ndivyo alivyoeleza msemaji huyo
Haikuweza kufahamika wazi ikiwa hatua
hiyo ya rais Putin ni jaribio la kuitekea baadhi ya wito wan chi za
magharibi kuutuliza mzozo huo ambao umeupa mtihani mkubwa mustakbali wa
Ukraine .
Kerry atua mjini Kiev
Hatua hiyo imekuja wakati Waziri wa
mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry akielekea Kiev kwa
mazungumzo na utawala mpya ambao umeshutumu Urusi kwa uvamizi wa
kijeshi. Ikulu ya Urusi ambayo haiutambui uongozi mpya mjini Kiev
inashikilia kwamba hatua yake ni kwa ajili ya kuwalinda mamilioni ya
Warusi wanaoishi Crimea.
Katika mjadala kwenye Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa jana , Balozi wa Urusi alisema kiongozi wa
aliyeondolewa madarakani Viktor Yanukovich aliiandikia barua Urusi
kuiomba ijiingize kijeshi kurejesha amani , sheria na utengamano.
Takriban wanachama wote wa baraza hilo
waliitaka Urusi kuyaondoa majeshi yake katika ardhi ya Ukraine, wito
ulioungwa mkono hata na mshirika wake China.
Mjini Washington, rais Barack Obama wa
Marekani aliita hatua ya Urusi kujiingiza kijeshi katika jimbo, la
Crimea kuwa ni ukiukaji wa sheria ya kimataifa. Obama akalitaka bunge
kuidhinisha mpango wa msaada kwa serikali ya Ukraine na kutoa tena
kitisho kwamba Marekani itachukua hatua kuiadhibu Urusi kiuchumi na
kuitenga kidiplomasia.
Obama aikosoa tena Urusi
Hata hivyo afisa mmoja wa Ikulu ya
Urusi mjini Moscow ameionya Marekani akisema vikwazo dhidi ya Urusi
akisema pindi ikifanya hivyo, mfumo mzima wa fedha wa Marekani
utaporomoka na Urusi itatafuta njia mbadala ya kutoitegemea marekani
hata kidogo.
Wakati huo huo pamoja na kwamba hali
ya mambo ni shwari kwa kiasi fulani katika jimbo la Ukraine la
Crimea,mapema leo watu waliokuwa na silaha wanaoiunga mkono Urusi huko
Crimea walifyatua risasi hewani kuwatawanya wanajeshi wapatao 300 wa
Ukraine ambao waliizingira kambi ya jeshi la anga ya Belbek,wakidai
warejeshwe kazini. Wanajeshi kadhaa wa Urusi walionekana wakiangalia tu
tukio hilo .
Chanzo, dw.de/Swahili
0 comments:
Post a Comment