Mgombea ubunge Jimbo la
Kalenga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa (32), akiwapungia wananchi huku
akiwa amebebwa alipowasili kwenye mkutano wa kampeni katika Kijiji cha
Mangalali, Kata ya Ulanda, Iringa Vijijini leo mchana.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM,
Mwigulu Nchemba akiongoza msafara wa mgombea ubunge wa Jimbo la Kalenga,
Godfrey Mgimwa aliyebebwa walipowasili kwenye mkutano wa kampeni katika
Kijiji cha Mangalali.
Mgimwa akiungana na
wanakijiji kucheza ngoma ya asili ya kabila la Wahehe alipowasili kwenye
mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Kibebe, Kata ya Ulanda mchana leo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM,
Nchemba (kulia), Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Joyce Msamba tavangu
(katikati) na mgombea ubunge kupitia CCM, Mgimwa wakicheza walipofika
kwenye kampeni katika Kijiji cha Kibebe.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO
BLOG
Vijana wakimkaribisha kwa kucheza kijana mwenzao Godfrey Mgimwa katika mkutano huo wa kampeni
Nani zaidi?
Mama mkazi wa Kijiji cha
Kibebe, Venanzila Kihaga akiwa ameshika kipeperushi cha Mgombea Ubunge
Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa, alipoteuliwa na wanakijiji kumuombea
kimila Mgimwa ashinde uchaguzi huo utakaofanyika Machi 16, mwaka huu.
Mchungaji wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania Usharika wa Kalenga Tosamaganga,Kisabugo
Mkemwa akitoa mahubiri ya kumuombea Mgimwa (kushoto) ili ashinde
uchaguzi huo. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Nchemba.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa
CCM Wilaya ya Iringa, Aloyce Mgongolwa akisikiliza kwa makini wakati
Nchemba akihutubia katika mkutano huo wa kampeni katika Kijiji cha
Kibebe.
Balozi wa CCM Tawi la Kibebebe, Julius Kihaga akiwa makini kusikiliza hotuba ya Mgimwa
Ofisa Mwandamizi wa
Mawasiliano wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Gabriel Athuman akinywa maji
ya kisima ambayo aliyasifia kuwa ni matamu wakati wa mkutano wa Kampeni
za CCM Jimbo la Kalenga katika Kijiji cha Kibebe
Akina mama wakisikiliza kwa makini wakati Mgimwa akijinaji katika mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Kibebe leo mchana.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Joyce Msambatavangu akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Kalenga, Mgimwa.
Aliyewahi kuwa Mgombea
ubunge Jimbo la Mbozi Mashariki kupitia Chadema, na Ofisa wa Chadema
Makao Makuu, Mwampamba akielezea jinsi alivyoamua kujiondoa kwenye chama
hicho bhaada ya kufanyiwa mabaya na uongozi wa Chadema ambacho alidai
hakifai wananchi kujiunga nacho.
PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
0 comments:
Post a Comment