Kundi la mataifa saba yaliyostawi
zaidi kiviwanda almaarufu kama G7 limelaani vikali hatua za kijeshi
zilizochukuliwa na Urusi nchini Ukraine-viongozi kundi hilo wakitaja
hatua ya Urusi kama ukiukaji wa uhuru wa Ukraine.
Katika taarifa ya pamoja iliyotiwa pia saini na Umoja wa Ulaya EU-Urusi imetakiwa kushughulia wasiwasi wake kuihusu Ukraini kupitia mashauri au upatanishi.
Katika taarifa ya pamoja iliyotiwa pia saini na Umoja wa Ulaya EU-Urusi imetakiwa kushughulia wasiwasi wake kuihusu Ukraini kupitia mashauri au upatanishi.
Kundi hilo la mataifa saba tajiri
zaidi duniani maarufu kama G-Seven limesema kuwa linachukuwa uamuzi wa
kuahirisha matayarisho ya kongamano ambalo lingefanyika nchini Urusi
mwezi juni mwaka huu kutokana na vitendo vya Moscow. Taarifa hiyo
inakuja wakati vikosi vya Urusi vikiimarisha uthibiti katika rasi ya
crimea ambapo Urusi inasema kuwa inalinda raia wake baada ya serikali
kupinduliwa mjini Kiev.
Mbunge mashuhuri wa Urusi - Vyacheslav
Nikonov, ameimabia BBC kwamba Urusi imejiandaa kwenda vitani kulinda
maslahi yake nchini Ukraine na hususan katika mji wa Sevastopol.
"Ukraine ilialikwa kujiunga na Nato na
hii ina maana kuwa marekani, au vituo vyake vya kijeshi vitawekwa
nchini Ukraine. Urusi itafanya lolote, itahatarisha kuingia vita kuzuia
hilo kutokea. Ni kuhusu kituo cha kijeshi, ni kuhusu mustakabal wa
Urusi, mustakabal wa Ukraine. Sidhani kama mataifa ya magharibi
yanaelewa kwamba Ukraine ni mahali ambapo Urusi ilizaliwa," amesema
Nikonov.
Awali serikali ya mpito ya Ukraine
iliishutumu Urusi kwa kutangaza vita na kuwaamuru wanajeshi wake kuwa
tayari kwa makabiliano.Shirika la kujihami kwa mataifa ya Magharibi NATO
limetowa wito kwa Urusi kuwaondoa wanajeshi wake nchini Ukrainena
kuzitaka pande zote kusuluhisha mgogoro huo kwa njia ya amani. Taarifa
hiyo imetolewa baada ya mkutano wa dharura wa mabalozi wa NATO mjini
Brussels kujadili mgogoro huo. Katibu mkuu wa NATO, Anders Fogh
Rasmussen, amesema kuwa huenda wachunguzi wa umoja wa mataifa wakatumwa
kusaidia kusuluhisha hali ya mambo.
"Tunatoa wito kwa urusi kuheshimu
ahadi zake za kimataifa, kuondoa vikosi vyake na kujiepusha na uvamizi
katika maeneo mengine nchini Ukraine. Tunatowa wito kwa pande zote
kufuata njia ya amani katika kusuluhisha mgogoro huo kupitia mazungumzo,
kupitia wachunguzi wa kimataifa chini ya mwavuli wa umoja wa baraza la
usalama la umoja wa mataifa au shirika la ushirikiano wa kiusalama ulaya
OSCE,'' amesema bwana Rasmussen.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni
wa marekani , John Kerry, anatarajiwa kuzuru Kiev hapo kesho jumanne
kuiunga mkono serikali mpya ya Ukraine.
Haya yanajiri wakati mkuu wa jeshi la
wanamaji wa Ukraine, Denis Berezovsky, akipokonywa madaraka yake baada
ya kusema hadharani kwamba anaunga mkono serikali mpya ya Jimbo la
Crimea ambayo inaunga mkono Urusi. Serikali ya Kiev imesema kuwa
inamfanyia uchunguzi kwa nia ya kumfungulia mashtaka ya uhaini.
Chanzo, bbcswahili
0 comments:
Post a Comment