HOME »
» NAIBU WAZIRI MALIASILI NA UTALII LAZARO NYALANDU AAGIZA KUMALIZWA KWA MIGOGORO YA MIPAKA BAINA YA WANANCHI;
 |
Naibu
Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiongea na Kamati za Ulinzi na
Usalama za Mikoa ya Manyara na Dodoma wakati wa kikao maalum cha kujadili
masuala ya migogoro ya mipaka katika Hifadhi ya Taifa Tarangire na Pori la
Akiba la Mkungunero wilayani Babati, Manyara |
 |
Mkuu
wa Mkoa wa Manyara Mhe. Elaston Mbwilo akisitiza jambo wakati wa kikao maalum
cha Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Dodoma na Manyara cha kujadili
masuala ya migogoro ya mipaka katika Hifadhi ya Taifa Tarangire na Pori la
Akiba la Mkungunero wilayani Babati, Manyara. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Dk. Rehema Nchimbi |
 |
- Sehemu
wa wajumbe waliokutana katika kikao maalum cha Kamati za Ulinzi na Usalama
za mikoa ya Dodoma na Manyara cha kujadili masuala ya migogoro ya mipaka
katika Hifadhi ya Taifa Tarangire na Pori la Akiba la Mkungunero wilayani
Babati, Manyara.
|
 |
Kutoka
kulia: Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu, Mkuu wa Mkoa
wa Manyara Elaston Mbwilo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wakifuatilia mada. |
 |
- Kutoka
kulia: Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi, Mkurugenzi wa Idara ya
Wanyamapori Profesa Alexander Songorwa na KatibuTawala wa Mkoa wa Dodoma Rehema Madenge wakifuatilia mada
zilizowasilishwa wakati wa kikao maalum cha Kamati za Ulinzi na Usalama za
mikoa ya Dodoma na Manyara cha kujadili masuala ya migogoro ya mipaka
katika Hifadhi ya Taifa Tarangire na Pori la Akiba la Mkungunero wilayani
Babati, Manyara.
|


 |
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu Serikali ameagiza kumalizwa
kwa migogoro ya mipaka baina ya Hifadhi ya Tarangire, Pori la Akiba la
Mkungunero na wananchi iliyodumu kwa muda wa takribani miaka kumi hadi
sasa.
Nyalandu amewataka wananchi wa vijiji vinavyopakana na hifadhi hizo
kuacha kuvamia maeneo yaliyotengwa kisheria kwani kwa kufanya hivyo ni kuleta
migogoro isiyo ya lazima.
Mhe.
Nyalandu alikuwa akiongea katika kikao maalum cha Kamati za Ulinzi na Usalama
za mikoa ya Manayara na Dodoma wilayani Babati mkoani Manyara zilizokutana kwa
ajili ya kujadili suluhu ya migogoro hiyo.
Aliongeza
kusema kuwa serikali imedhamiria kumaliza mgogoro hiyo kwa kuishirikisha jamii
kwa upana zaidi huku akisisitiza kwamba Serikali itaendelea kusimamia na
kutekeleza Sheria ya Uhifadhi bila kumuonea mwananchi yoyote na kwa kuzingatia
haki za binadamu.
|
0 comments:
Post a Comment