Musley Al Rawahi
akisisitiza jambo.
Mjumbe mpya wa kamati ya
utendaji wa klabu ya Simba, Musley Al Rawahi, amesema kuwa silaha kubwa ya
kufikia maendeleo katika klabu hiyo ni umoja na kufanya kazi kwa kujituma na
uadilifu mkubwa.
Musley ambaye mwaka jana
alimzawadia gari kiungo wa Simba SC, Ramadhani “Messi” Singano kwa kucheza
vizuri katika ligi kuu ya Tanzania Bara, alisema hayo mara baada ya
kutangazwa kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu hiyo na pia kuwa miongozi
mwa wajumbe wanaounda kamati ngumu na nyeti ya usajili wa klabu hiyo.
Alisema kuwa anashukuru
kuteuliwa kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji na usajili wa klabu hiyo na
anaamini uteuzi wake umetokana na jinsi alivyokuwa mstari wa mbele kutafuta
maendeleo ya klabu hiyo.
Kwa mujibu wa Musley, Rais
wa klabu hiyo, Evans Aveva hajafanya makosa katika uteuzi wa wajumbe wa kamati
ya utendaji, usajili, mashindano na soka la vijana kwani hizo ndizo nguzo za
ustawi wa klabu na kufanikisha mambo mengi ya maendeleo.
“Tukisajili wachezaji
wazuri, ndiyo watatuletea ushindi ndani ya klabu na hivyo kamati ya mashindano
kufanyakazi zake kwa ufanisi mkubwa, hivyo natoa wito kwa wajumbe wateule,
tufanye kazi kwa bidii na kuleta maendeleo makubwa klabuni na kuendelea kumpa sifa
waliotuteua kushika nadhifa hizo,” alisema Musley.
Alisema kuwa yeye ana
historia kubwa sana katika klabu hiyo na amekuwa mwanachama tangu akiwa mdogo
na hiyo ilitokana na mapenzi makubwa ya baba yake kwa Simba.
“Mzee wangu amekuwa
mwanachama wa klabu hii kwa miaka mingi, mimi nimefuata nyayo zake na mpaka
sasa nimekuwa na klabu hii kwa miaka mingi, nina uchungu nayo sana, ninaahidi
kufanya kazi kwa bidii ili kufikia lengo,” alisema Musley.
Alisema kuwa changamoto
kubwa wanayokabiliana nayo ni matarajio ya wanachama na mashabiki wa Simba
kwani wanachotaka wao ni ushindi na kutwaa ubingwa.
“Wana-Simba wanataka
ubingwa, hakuna kingine ambacho wanakitaka, tunahitaji kusajili wachezaji
wazuri, wenye kuleta ufanisi na kutufikisha kule tunakotaka,” alisema.
Na Mwandishi wetu
0 comments:
Post a Comment