Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Imechapishwa Julai 22, 2014, saa 10:48 jioni
Kikosi
cha Taifa Stars kinatarajia kuondoka keshokutwa (Julai 24 mwaka huu)
kwenda Mbeya ambapo kitapiga kambi ya wiki moja kujiandaa kwa mechi ya
marudiano dhidi ya Msumbiji.
Mechi
hiyo ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kutafuta tiketi ya
kushiriki Fainali za Afrika (AFCON) zitakazochezwa mwakani nchini
Morocco itafanyika wikiendi ya Agosti 2 na 3 mwaka huu nchini Msumbiji.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaondoka nchini
Julai 31 mwaka huu kwenda Johannesburg, Afrika Kusini ambapo itafanya
mazoezi ya mwisho kabla ya kutua Maputo kwa ajili ya mechi hiyo
itakayochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimpeto.
Wakati
huo huo, mechi ya michuano ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na
Msumbiji (Mambas) iliyochezwa juzi (Julai 20 mwaka huu) imeingiza sh.
158,350,000 kutokana na washabiki 19,684 walioingia kwa kiingilio cha
sh. 7,000 na sh. 30,000.
Mgawo
wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) sh. 24,155,084.75, gharama za tiketi (MaxMalipo) sh. 19,684,000,
gharama za mchezo sh. 22,902,183, uwanja sh. 11,451,092, Shirikisho la
Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 5,725,546 na Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) sh. 74,432,095.
Tunawashukuru
washabiki wote waliojitokeza kwenye Uwanja wa Taifa kuishangilia Taifa
Stars katika mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya mabao 2-2.
0 comments:
Post a Comment