KUELEKEA MAZIZINI MPAKA MOSHI BAR
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya
Ilala Jerry Silaa Jana amefanya ziara fupi ya ukaguzi wa
ujenzi wa barabara ya ukonga Moshibar
ujenzi wa barabara ya ukonga Moshibar
kilometa 3 kiwango cha changalawe awamu yakwanza. Ikiwa ni
utekelezaji wa miradi ya
utekelezaji wa miradi ya
dharura kulingana na uharibifu wa miundo mbinu ulitokea baada
ya mvua kubwa.
ya mvua kubwa.
Mradi huo
ambao unaghalimu kiasi cha shilingi millioni 90.Pesa za
Ujenzi huo zinatoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.Pia Barabara hiyo
itawekwa Lami kwa awamu ya pili ndani ya mwaka huu kwa kilomita tatu.Picha Zote Na Dj Sek Blog
Ujenzi huo zinatoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.Pia Barabara hiyo
itawekwa Lami kwa awamu ya pili ndani ya mwaka huu kwa kilomita tatu.Picha Zote Na Dj Sek Blog
Mstahiki
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa wa Kwanza kushoto
akiwa na Mhandisi wa Barabara(mwenye shati Jeusi) pamoja na Diwani wa
ukonga Elizabeth Mbano(katikati) na wa kwanza Kulia ni Mhandisi wa
Manispaa Bwana Muhinda Kassimu wakitazama maendeleo ya ujenzi wa kipande
cha barabara kutoka ukonga-mazizini mpaka moshi bar.
Mhandisi
wa Manispaa Bwana Muhinda Kassimu Akielezea namna ambavyo awamu ya
kwanza ya ukarabati wa barabara hiyo utakavyo kuwa kwa kiwango cha
changarawe na itafuata awamu ya pili ambayo ni Lami.
Diwani
wa ukonga Elizabeth Mbano akiongea na vyombo vya habari kushukuru
Manispaa kwa kuikumbuka barabara hiyo kwani imekuwa ikileta sana shida
ya usafiri kwa wakazi wa eneo hilo hasa kipindi cha mvua.
Mstahiki
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa Akielezea namna
Barabara hiyo itakavyotengenezwa na pia akasisitiza kwamba Pesa za
Ujenzi wa Barabara Hiyo zimetoka ndani ya manispaa na si Vinginevyo.
Greda likirekebisha Barabara ya Ukonga-mazizini kulekea moshi bar
Mwonekano wa Bara barabara hiyo
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akimwelezea mkazi wa mazizini namna mradi wa barabara hiyo ulivyo.
Mstahiki
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akimuelezea kwa
kumuonyesha mkazi wa mazizini gharama za mradi huo na pia pesa za mradi
huo kutoka ndani ya Halmashauri na si vinginevyo.
Mstahiki
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwa amempa
nafasi mkazi wa Mazizini kupitia majalada yenye maelezo na mikataba ya
ujenzi wa barabara hiyo
Mstahiki
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiongea na wakazi
wa mazizini waliotaka kujua mradi utachukua mda gani na utaisha lini.
0 comments:
Post a Comment