Wataalamu wa kilimo wilayani
Handeni katika mkoa wa Tanga, leo watakutana kuweka mezani mapendekezo
ya mazao mapya yatakayofaa kwa biashara kwa lengo la kuinua kipato cha
mwananchi mmoja mmoja wilayani humo.
Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Muhingo
Rweyemamu, amesema leo kuwa katika mkutano huo, wataalamu hao watapitia
itifaki mbalimbali zilizofikiwa na kuanisha zao mbadala kwa biashara
kati ya korosho na ufututa ama yote mawili badala ya kutegemea mahindi
pekee kwa chakula na biashara.
Amesema kwa muda mrefu
imebainika kuwa pamoja na kuwa zao la mahindi hulimwa sana wilayani
humo, zao ambalo limekuwa halibadilishi hali ya uchumi kwa wakazi wa
wilaya hiyo kwa vile zao hilo pia hutumika kwa chakula jambo ambalo
amesema kama mwananchi ataamua kuuza kwa upande mwingine hukaribisha baa
la njaa katika kaya yake.
Amesema kubatikana kwa zao
mbadala kutawawezesha wananchi kuondokana na umasikini na wakati huo huo
kuendelea kubaki na chakula cha kutosha hadi msimu mwingine wa kilimo
tofauti na ilivyo sasa ambapo wananchi walio wengi huuza chakula chote
ili kupata mahitaji mengine huku wakibaki bila chakula majumbani hadi
kupelekea kuomba msaada serikalini.
0 comments:
Post a Comment