Viungo mbali mbali vya binadamu
vimekutwa katika eneo la kutupa taka la Bunju mjini Dar es Salaam katika
mazingira ambayo haijafahamika mara moja kuwa viungo hivyo vimetoka
wapi.
Kwa mjibu wa Afisa mmoja wa polisi ambaye
hakutaka jina lake litajwe amesema viungo hivyo vya binadamu
vilivyokutwa ni miguu,vidole ambavyo vilikutwa vikiwa vimefungwa ndani
ya mifuko.Mtu mmoja anashikiliwa kuhusishwa na tukio hilo ambaye ni dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo lililobeba viungo hivyo vya binadamu.
Haijafahamika mara moja miili hiyo ya binadamu imetolewa wapi na ilipelekwa eneo hilo kwa lengo gani.
Katika miaka ya hivi karibuni Tanzania imekuwa ikikabiliwa na tatizo la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi au Albino ambapo viungo vyao huchukuliwa,japo kuwa viungo hivi vilivyokutwa kwa sasa bado havihusishwi moja kwa moja na matukio ya mashambulizi na mauaji ya walemavu hao.
0 comments:
Post a Comment