Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais-Mazingira Mh. Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge akipata maelezo
kutoka kwa Afisa Mazingira wa Wilaya ya Ilala bw. Abdon Mapunda (wa pili
kushoto) alipotembelea bwawa la maji taka la Vingunguti jijini Dar es
Salaam.
Maji machafu yanayotoka katika
viwanda mbalimbali vilivyopo Vingunguti jijini Dar es Salaam ambayo
hutiririsha maji yake katika mto wa msimbazi, maji ambayo yanahatarisha
afya ya binadamu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais-Mazingira Mh. Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge (wa katikati)
akizungumza na Menejimenti ya kiwanda cha kuzalisha mafuta ya kupikia
(Murza Oil Mills Limited) kilichopo vingunguti jijini Dar es Salaam,
wakati wa ziara yake ya kukagua mazingira katika kiwanda hicho na
kuwataka watumie mfumo sahihi wa maji taka ili kulinda mazimgira na
kuepuka athari mbalimbali kwa wananchi.
Meneja wa kiwanda cha Murza Oil
Mills Limited Bw. Dinesh Kana (wa tatu kushoto) akitoa maelezo kwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Mh. Dkt. Injinia
Binilith Satano Mahenge (wa nne kushoto) kuhusu mfumo wa maji taka ambao
wanautumia katika kiwanda hicho.
sehemu ya dampo la Pugu Kinyamwezi lilopo jijini Dar es Salaam
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais-Mazingira Mh. Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge akipata maelezo
kutoka kwa Bw. Richard Matari ambaye ni msimamizi wa dampo la Kinyamwezi
lililopo Pugu jijini Dar es Salaam, baada ya waziri kuwasili katika
dampo hilo na kutaka kujua utendaji wa kazi zao katika kulinda
Mazingira.
………………………………………………………………………….
Na Rashda Swedi- VPO
Viwanda vitakavyokiuka masharti na
kanuni za kulinda mazingira havina budi kufungiwa mpaka vitakapofuata
taratibu na sheria za utunzaji wa Mazingira.
Hayo yamesemwa hivi karibuni
jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais –
Mzingira Mh. Dkt. Injinia Binilith Mahenge alipofanya ziara fupi ya
kutembelea kiwanda cha kuzalisha mafuta (Murza Oil Mills Limited)
kilichopo Vingunguti.
hata hivyo Mheshimiwa Mahenge
alisema hayo baada ya kutoridhishwa na mfumo wa maji taka ya kiwanda
hicho na kuwaambia waboreshe zaidi mfumo wa maji taka kwa lengo la
kulinda mazingira kwa sababu wasipofanya hivyo Serikali itachukua hatua
ya kukifunga kiwanda hicho.
wakati huo huo, mwanasheria wa
NEMC Bw.Manchale Heche amesema kuwa, kutokana na ziara waliyoifanya
pamoja na Mh. Waziri wamegundua mengi na hawatafumbia macho suala la
viwanda vinavyotumia magogo,kuni na wale wasiokuwa na mfumo mzuri wa
majitaka endapo hawatafuata masharti waliyokubaliana nayo viwanda hivyo
vitafungiwa.
Aidha, Waziri alitembelea pia
bwawa la maji taka lililopo Vingunguti jijini Dar es Salaam na kugundua
kuwa kuna uharibifu mkubwa wa Mazigira, kutokana na maji machafu
yanayotoka katika viwanda mbalimbali karibu na eneo hilo kutiririsha
maji yao kwenye mabwawa hayo.Kutokana na hilo amewataka Manispaa
kushirikiana na NEMC kuvijua viwanda vinavyopitisha maji machafu moja
kwa moja bila kufuata utaratibu uliowekwa.
“Ni wajibu wa kila mtu kulinda
mazingira na sio wajibu wa Ofisi ya makamu wa Rais tu kwani Mazingira ni
yetu sote na ni muhimu kuyalinda” Mh. Mahenge alisema.Alisisitiza kuwa,
huo hautakuwa mwisho wa ukaguzi wa viwanda utaratibu wa kukagua viwanda
utaendelea kuangalia Mazingira rafiki kwa wananchi.
0 comments:
Post a Comment