Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akihutubia wajumbe wa Chama cha Wabunge kutoka nchi za Jumuiya ya Madola
(CPA) katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha.
Mheshimiwa Makamu wa Rais alifungua mkutano wa 45 wa CPA unaozikutanisha
nchi za Afrika unaofanyika nchini Tanzania kuanzia leo Julai 24 hadi
Julai 27, 2014. Mkutano huo sambamba na masuala mengine pia unajadili
juu ya wajibu wa mabunge na mchango wao katika kusimamia utawala bora
pamoja na kusaidia serikali za Afrika kubuni mipango ya maendeleo
inayolenga vizazi vya sasa kwa lengo la kuijenga Afrika ijayo. Picha na
OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na Makamu wa Rais wa CPA na Spika wa Ufalme wa Lethoto, Enoch
Sephir Motanyane, wakati akiondoka nje ya ukumbi wa AICC baada ya
kufungua rasmi mkutano wa 45 wa CPA unaozikutanisha nchi za Afrika
unaofanyika nchini Tanzania, jijini Arusha kuanzia leo Julai 24 hadi
Julai 27, 2014. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na baadhi ya Wabunge wakati akiondoka nje ya ukumbi wa AICC
jijini Arusha baada ya kufungua rasmi mkutano wa 45 wa CPA
unaozikutanisha nchi za Afrika unaofanyika nchini Tanzania, kuanzia leo
Julai 24 hadi Julai 27, 2014. \
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
Spika wa Bunge la Jamhuri, Anne Makinda na Mwenyekiti wa CPA Tawi la
Tanzania, Azan Zungu, wakifurahia ngoma ya asili ya kabila la kimasai
wakati walipokuwa wakiwasili kwenye ukumbi wa AICC, jijini Arusha
kufungua mkutano wa 45 wa CPA unaozikutanisha nchi za Afrika unaofanyika
nchini Tanzania, kuanzia leo Julai 24 hadi Julai 27, 2014. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wabunge baada ya
kufungua rasmi mkutano wa 45 wa CPA unaozikutanisha nchi za Afrika
unaofanyika nchini Tanzania, kuanzia leo Julai 24 hadi Julai 27, 2014.
Picha na OMR
0 comments:
Post a Comment