Sunday, 27 July 2014

UJIO WA REAL MADRID TANZANIA SASA YAWA GUMZO NCHINI


FIGO


Gumzo la ujio wa wakongwe wa Real Madrid sasa umeanza kuwa gumzo kuliko hata ilivyotarajiwa awali.
Mwanzo ilionekana kama wengi hawaamini kama kweli wakongwe hao wa Madrid wanaweza kuja nchini.
Baadhi wametuma baruapepe kwenye mtandao huu wakihoji kama ni kweli.
Wengine walitaka kujua kama kweli wachezaji kama Luis Figo au Raul Gonzalez wanaweza kukanyaga ardhi ya Tanzania.
“Maandalizi yanaendelea vizuri kama tulivyosema awali na watu wanapaswa kuamini kuwa kweli Madrid wakongwe wanakuja.
“Hii ni nafasi kubwa kwa Watanzania kukutana na nyota hao na kuwaona wanacheza, hivyo wajiandae kupata burudani hiyo,” alisema Ssebo ambaye ni mratibu wa ziara hiyo.
Wakali hao watakipiga na nyota wa Tanzania ambao watajumuishwa pamoja katika mechi itakayopigwa Agosti 23 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salam.

0 comments: