Thursday, 24 July 2014

YANGA YASEMA HAIJAJITOA KAGAME:



Klabu ya Young Africans haijajitoa kushiriki mashindano ya Kombe la Kagame chini Rwanda kama inavyoripotiwa na baadhi ya mitandao ya habari nchini na kusema taarifa hizo ni za uongo.

Katibu mkuu wa Yanga SC Bw Beno Njovu amesema taarifa hizo zilizosambazwa ni za uongo na kuwa kwa siku ya leo hajaongea na mwandishi wa habari yoyote juu ya michuano hiyo.

Sie hatujatangaza kutoshiriki michuano ya Kagame, kama tulivyosema awali kikubwa tunasubiri taarifa rasmi za kushiriki kutoka CECAFA zitufikie ofisini nasi tupange mikakati yetu "amesema Beno".

0 comments: