Tuesday, 22 July 2014

TETESI ZA USAJILI: MAN U YAIMARISHA MAMBO KUMNASA ARTURO VIDAL WA JUVENTUS


Manchester United to launch new €54m Vidal bid
 

MANCHESTER United wiki hii wapo tayari kuanza kuifukuzia saini ya kiungo wa Juventus, Arturo Vidal kwa dau la Euro milioni 54.
Klabu hiyo ya Old Trafford imejiamini kuwa itamnasa nyota huyo wa Chile katika fainali za kombe la dunia na wanaanza harakati zaidi kumuwinda kiungo  huyo mwenye miaka 27.
Louis Van Gaal ambaye alitambulishwa rasmi kuanza kazi jumatano ya wiki iliyopita, ni shabiki mkubwa wa Vidal na aliwahi kujaribu kumsajili alipokuwa anafanya kazi Bayern Munich mwaka 2011 na amethibitisha kumhijtaji tena.
Mholanzi huyo alijaribu kumshawishi Vidal mapema mwezi Julai, licha ya klabu yake kuambiwa kuwa itawagharimu Euro milioni 56 jumlisha Luis Nani.
Juventus wamemsajili Alvaro Morata kutoka Real Madrid na wanapambana kumnasa Roberto Pereyra, wakati huo huo inapendekezwa kuwa Vidal auzwe ili kupata hela.
Vidal ambaye kwasasa anapumzika nchini Chile kufuatia kumalizika kwa fainali za kombe la dunia, hivi karibuni alisema hatima yake Turin ipo mashakani.
“Sidhani kama muda wangu Juventus umekwisha, ingawa siwezi kusema kwasasa,” aliiambia Radio ya Chile. “Nitakaporudi kutoka Chile, nitazungumza na mabosi wangu na tutaona kitakachotokea”.
Mkurugenzi wa Juve, Pavel Nedved alisema klabu inaona ugumu kuwauza Vidal na Pogba, lakini alikiri dau kubwa linaweza kuwalazimisha kufanya biashara.
‘Mipango yetu ipo wazi, tunataka kuwabakisha wachezaji wote muhimu wakiwemo Vidal na Pogba,” . Aliwaambia Tuttospot. “Hatudhani kama tutauza mchezaji yeyote hususani Vidal”.

‘Lakini kama kuna dau kubwa, tunaweza kulifikria hilo, lakini hatutaki kuuza mabingwa wetu”.

OFFICIAL: LIVERPOOL YAMTOA KWA MKOPO IAGO ASPAS SEVILLA

Imechapishwa Julai 21, 2014, saa 10:03 jioni

 LIVERPOOL imethibitisha kumtoa kwa mkopo,  Iago Aspas katika klabu ya Sevilla ili aicheze kwa msimu wa 2014/2015.
Mshambuliaji huyo alijiunga na wekundu wa Anfield kutoka CeltaVigo majira ya kiangazi mwaka jana, lakini ameshindwa kuingia timu ya kwanza na amecheza mechi 15 katika mashindano yote.
Sevilla alitangaza kukamilika kwa dili hilo wiki iliyopita na kusema kuwa watafanya mpango wa kumsajili kwa mkataba wa kudumu mchezaji huyo mwenye miaka 26.
Nafasi yake katika klabu imedhoofishwa zaidi na Brendan Rodgers baada ya kumsajili Adam Lallana, Rickie Lambert na Lazar Markovic, japokuwa Luis Suarez ameuzwa.
Aspas aliifungia Liverpool goli pekee katika mchezo wa raundi ya tatu ya kombe la FA mwezi januari.
Lucas Leiva naye anatarajia kuondoka Anfield kwa mkopo na kujiunga na Napoli ambayo inakaribia kumsajili kiungo huyo wa Brazil.

Pia Liverpool wamekubali kumuuza Fabio Borini katika klabu ya Sunderland na kichobaki ni makubaliano binafsi na mchezaji.

0 comments: