WAKATI hamu ya mashabiki kila kona
kwa sasa ni Agosti 8, mwaka huu katika tamasha kubwa la kihistoria la
Usiku wa Matumaini litakalofanyia Uwanja wa Taifa jijini Dar, mashabiki
wengi wanatamani kuwaona wakali kibao wakipanda jukwaani na kupiga
nyimbo zao kali.
Diva wa muziki kutoka Nigeria anayetamba na wimbo wa Johnny, Yemi Alade
Good newz ni kwamba Zuwena Mohamed
‘Shilole’ atapanda jukwaa moja na diva wa muziki kutoka Nigeria
anayetamba na wimbo wa Johnny, Yemi Alade kudondosha shoo ya kihistoria.
Uzuri wa wasanii hao wawili ndiyo unashawishi watu wengi
kufika katika tamasha hilo lenye lengo ya kuchangia mfuko wa elimu
nchini. Unataka kujua sifa za wasanii hao? Hizi hapa:
Shilole ambaye wengi wamezoea
kumwita Shishi Baby, amekuwa habahatishi jukwaani kwa jinsi anavyojua
kuwapagawisha, hivyo mashabiki wategemee sapraizi kibao kutoka kwa
bidada huyo kwenye sekta maalum ya kukata mauno na kuacha watu midomo
wazi.
Kwa upande wake, Yemi Alade
anatisha balaa. Staili ya Johnny ndiyo atakayoinesha siku hiyo huku
akichungulia kwa kumtafuta Johnny uwanjani mpaka atakapofanikiwa kumuona
na kurudi naye Nigeria kama alivyoahidi.
NGOMA ZAO
Pata picha kwa Shilole atapopanda na kupiga nyimbo zake kali
kama Chuna Buzi, Lawama, Nakomaa na Jiji, Paka la Baa na Namchukua
inayotamba kwa sasa, hakika patakuwa hapatoshi kwani Shilole amesema
hatabakisha kitu siku hiyo.
Zuwena Mohamed ‘Shilole’
Bidada Yemi Alade atashuka na
ngoma inayotamba Afrika, Johnny kisha atazidondosha kali nyingine ambazo
zimetokea kuiteka Afrika kama GhenGhenLove, Bamboo, Show Me na
Tangerine.
MADANSA
Shilole ameahidi kudondoka na madansa wake ambapo watakuwa naye sambamba jukwaani katika kukamua siku hiyo.
“Mashabiki wategemee kuona
mpangilio na staili tofauti kutoka kwa masteji shoo hao ambazo zitakuwa
funika bovu,” alisema Shilole.
Yemi naye hatakuwa nyuma katika
eneo hilo, ameahidi kucheza sambamba na madansa wake siku hiyo. Kama
ilivyo kwenye makamuzi yake kupitia video ya Johnny na Tangerine ambapo
madensa wake wanaonekana wakikamua mwanzo mwisho.
WENGINE
Mratibu wa tamasha hilo, Luqman Maloto amefunguka kuwa mbali
na shoo hiyo kali, utamu zaidi utakolezwa zaidi na mastaa wakali wa
Bongo Fleva wakiongozwa na mfalme, Saleh Ally ‘Ali Kiba’, Meninah,
Madee, R.O.M.A Mkatoliki, Scorpion Girls, Juma Nature na kundi zima la
TMK Wanaume Halisi.“Kila msanii atakayepanda jukwaani atahakikisha anapiga nyimbo zake zote ndipo ampishe mwenzake, itakuwa ni jiwe baada ya jiwe,” alisema Maloto.
Aidha, tamasha hilo litapambwa na
mechi za mpira wa miguu kati ya wabunge mashabiki wa Simba na wenzao wa
Yanga, Bongo Fleva na Bongo Movie pamoja na mapambano kibao ya ndondi,
burudani zote hizo mashabiki watazipata kwa kiingilio cha shilingi elfu
tano.
Tamasha hilo limedhaminiwa na E.FM, Clouds FM, Times FM, Vodacom, Pepsi, Azam TV na SYSCORP.
JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS
0 comments:
Post a Comment