Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali
Ngemela Lubinga akifungua kikao mkutano mkuu wa mwaka wa baraza la
madiwani Halmshauri ya NSIMBO Mbele ya wajumbe wa kikao hicho pamoja na
watalaam wa Halamshauri hiyo
……………………………………….
Na Kibada Kibada –Nsimbo Katavi.
Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali Ngemela Lubinga amewataka
madiwani kusimamia kwa ukaribu miradi mbalimbali ya maendeleo katika
maeneo yao kwa kuwa wao wana dhamana kubwa katika jamii wanayoingoza
kama wawakilishi wa wananchi kwenye Vikao vya maamuzi hivyo ni wajibu
wao kutimiza wajibu huo.
Kanali Lubinga aliyasema hayo wakati akifungua kikao cha Mkutano
Mkuu wa Mwaka wa Fedha uliokwisha wa 2013/2014.na kueleza kuwa
uwakilishi ni dhamana kubwa katika jamii ambayo ni wananchi
unaowawakilishi hivyo wanatakiwa kuwatendea haki kwa kutimiza wajibu
wako waliokabidhiwa katika jamii ya uwakilishi ikiwa ni pamoja na
kusimamia kwa umakini utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyoko kwenye
Halmashauri katika eneo husika.
Alisema matatizo yaliyoko kwenye eneo la diwani unatakiwa
kuyatambua na kuyapatia maamuzi mfano wizi unatokeo kwenye eneo lako
kama wizi wa Soral Kijiji cha Ugala pale upo uongozi upo kuanzia ngazi
ya Kijiji,Kata na Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo katika Kata ni
Diwani na wataalamu wake wapo pia na Diwani yupo katika eneo , kweli
kama upo uwajibikaji na kutimiza wajibu wananchi wangeweza kutoa
ushirikiano na mali kama hiyo isingeibiwa kwa kuwa wanaona ni mali ya
jamii kwa manufaa ya jamii lazima watailinda kwa gharama yeyote ili ila
kama hakuna uwajibikaji na ushirikiano basi wananchi hwawezi kutoa
ushirikiano..
Akasema siwajibu wa viongozi kuktaa watu bali wanasimamiwa
ukiwasimamia kwa ukaribu matatizo yaliyopo kwenye eneolako utayafahamu
na kutafuta njia ya kuyapatia ufumbuzi kabla hayajawa makubwa .
Akizungumzia suala la ujenzi wa Maabara alieleza kuwa
Halmashauri ya Nsimbo iko nyuma katika utekelezaji wa agizo la Rais na
agizo la Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe lakuzitaka
halmashauri zote kukamilisha ujenzi wa Maabara kwa shule za Sekondari
ifika mwezi Novemba hali ya ujenzi inakwenda kwa kusuasua mno tofauti na
maeneo mengine katika Mkoa.
Mkuu huyo wa wilaya ameitaka Halmashauri kuwatumia na kutumia
fursa zilizopo katika Hlamshauri hiyo hasa makampuni ya uchimbaji madini
nay ale ya nayojishughulisha na unuzi wa tumbuka kuhakikisha
wanawashirikisha wasaidie katika ujenzi wa Maabara.
Akasisitiza kuwa Mkoa wa Katavi na Halmashauri ya Nsimbo
wanaoutajiri wa kutosha watumieni hawa watu waweze kuwasidia katika
kujenga maabara hizo hawa wanachuma mali kwenye halmashauri yetu
haiwezekana na wao wasisaidie watalaam tumieni Talaam zenu kuwasiadia
wananchi hao.
Akasema hataki kusikia shule hazina madawati katika Wilaya yake
na ameisha agiza mamlaka inayohusika kutoa kibali au leseni ya kuvuna
kupasua mbao katika Wilaya yake mvuna huyo lazima achangie madawati 300
hiyo ni lazima kwa kuwa ni agizo lasivyo asipewe leseni hiyo ya kupasua
mbao kama hataki kuchangia madawati hayo.
Katika hatua nyingine amewaagiza watendaji wa Halmashauri hasa
Idara ya utumishi kuondoa kero na manunguniko kwa watumishi
wanaolalamikia kututendewa haki kwa kulipwa masilahi yao nap engine
posho zao akasema iwapo malalamiko yatazidi watu watachukia na kuichukia
serikali yao vita ya namna hiyo siyo lahisi kuishinda ni vyema watu
wakasilikizwa na kupewa haki zaowanazodai kama madai yao mbalimbali
katika Halmashauri.
Kwa upande wake Mweyekiti wa Halmashauri ya Nsimbo Mohamed
Assenga alieleza kuwa kuwa kwa kuwa wote ni viongozi watajitahidi
kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ili kuhakikisha
maendeleo katika Halmashauri yanakwenda kama inavyotakiwa kwa kuwaletea
wananchi maendeleo kwa mstakabali wa Taifa.
Katika kikao hicho ambacho kilikuwa ni Mkutano Mkuu wa mwisho wa
Mwaka wa fedha unaoishia 2013/2014 Taarifa mbalimbali za utekelezaji wa
miradi ya maendeleo na shughuli nyingine ziliwasilishwa na kujadiliwa
na kupatiwa majibu.
0 comments:
Post a Comment