MSHAMBULIAJI
wa kimataifa wa England, Wayne Rooney amemdhihirishia ubora wake kocha
mpya wa Manchester United, Mholanzi Louis van Gaal usiku huu baada ya
kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-2 dhidi ya AS Roma mjini
Denver, Marekani.
Katika
mchezo wa kujianda na msimu, Rooney alifunga katika dakika za 36 na 44
kwa penalti, wakati bao lingine la United lilifungwa na Juan Mata dakika
ya 39.
Mabao ya Roma yalifungwa Miralem Pjanic dakika ya 75 na mkongwe Francesco Totti kwa penalti dakika ya 88.
La kwanza: Rooney alifunga bao la kwanza kutoka umbali wa mita 25 mjini Denver
Yuko vizuri: Juan Mata alifunga bonge la bao kipindi cha kwanza
Mechi
hiyo iliyochezeshwa na refa Allen Chapman mbele ya mashabiki 54,117,
Rooney aliibuka mchezaji bora baada ya filimbi ya mwisho.
Kikosi
cha Manchester United kilikuwa; Johnstone/Amos dk45, Blackett, Jones/M
Keane dk45, Evans/Smalling dk45, Valencia/Young dk45, Herrera/Nani dk45,
Cleverley/Hernandez dk69, Mata/Kagawa dk45, James/Shaw dk45, Rooney/W
Keane dk45 na Welbeck/Lingard dk45.
AS
Roma; Skorupski, Calabresi/Somma dk45, Benatia, Romangnoli/Castan dk45,
Emanuelson/Cole dk45, Ucan, Keita/Pjanic dk68, Iturbe/Ljajic dk45,
Paredes/Nainggolan dk45, Florenzi/Totti dk6 na Destro
Tuta: Rooney akifunga kwa penalti
Rooney akigombea mpira na Mattia Destro
0 comments:
Post a Comment