KOCHA wa zamani wa Chelsea, Claudio Ranieri ameteuliwa kuifundisha Ugiriki, Shirikisho la Soka la nchi hiyo limesema.
Babu
huyo Mtaliano mwenye umri wa miaka 62 anakwenda kurithi mikoba ya
Fernando Santos, ambaye amemaliza mkataba wake baada ya Fainali za Kombe
la Dunia, akiifikisha Ugiriki katika hatua ya 16 Bora.
Ranieri
amepewa mkataba wa miaka miwili na sasa atakuwa na jukumu la kuiwezesha
Ugiriki kufuzu kwenye Fainali za Euro mwaka 2016.
Mechi
ya kwanza ya Ranieri itakuwa ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Ulaya
dhidi ya Romania Septemba 7 na baadaye dhidi ya Ireland Kaskazini,
Hungary, Finland na Visiwa vya Faroe alizopangwa nazo katika Kundi F.
Mkongwe
huyo amekuwa 'juu ya maws tangu alipofukuzwa Monaco Mei baada ya
kupiga kazi kwa misimu miwili. Ranieri alitengeneza jina lake nchini
kwao aliposhinda taji la Coppa Italia akiwa na Fiorentina kabla ya
kutimkia Valencia, ambako alitwaa Copa del Rey na Kombe la Intertoto.
Akaenda
kupiga kazi misimu minne Chelsea kabla ya kurejea kwa muda Valencia na
kisha kupiga kazi Parma, Juventus, Roma na Inter Milan.
0 comments:
Post a Comment