Imechapishwa Julai 22, 2014, saa 11:02 jioni
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeongeza muda wa usajili kwa wiki
mbili ili kuzipa klabu nafasi ya kukamilisha taratibu zinazotakiwa.
Hivyo hatua ya kwanza ya usajili inakamilika Agosti 17 mwaka huu badala
ya Agosti 3 ya awali.
Kutokana
na marekebisho hayo, kipindi cha uhamisho kinakamilika Agosti 17 mwaka
huu wakati pingamizi itakuwa kati ya Agosti 19 hadi 26 mwaka huu.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itathibitisha usajili kati ya Septemba 1 na 2 mwaka huu.
Uhamisho
wa kimataifa, usajili wa wachezaji huru, na utatuzi wa dosari za
usajili unatakiwa uwe umekamilika kufikia Septemba 7 mwaka huu.
Uthibitisho wa hatua ya mwisho ya usajili utafanywa Septemba 15 mwaka
huu.
Kwa
upande wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2014/2015 itaanza Septemba
20 mwaka huu, na ratiba itatolewa mwezi mmoja kabla ya kuanza ligi
hiyo.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF
0 comments:
Post a Comment