Vyombo vya usalama vya Marekani
vimesema havina ushahidi wa kuihusisha moja kwa moja serikali ya urusi
kuhusika katika kuidondosha ndege ya abiria ya Malaysia huko mashariki
ya Ukraine.
Lakini wanasema huenda waasi wa urusi waliiangusha Boeing 777 kimakosa.Ili kujua kilichotokea, waangalizi wa ulaya wa masuala ya kiusalama wameendelea kulichunguza eneo ilipoangukia ndege ambalo ni eneo linaloshikiliwa na waasi.
Msemaji wa shirika hilo Michael Borchokyo amesema uchunguzi walioufanya kwa siku tano umewafanya kugundua mambo kadhaa ikiwamo kusogezwa pembeni kipande kikubwa cha ndege hiyo kitumikacho kubeba mizigo na abiria.
"Tumegundua kuna mambo yamefanywa katika eneo la tukio, takribani mambo nane hivi. Hasa kwenye eneo hasa ndege yenyewe ilipoangukia. Tumetizama kama siku mbili zilizopita tukagundua ni kama kipande kilikatwa hivi. Hatuwezi kuthibitisha kwa hakika pengine likuwa katika kutafuta miili hatuna hakika" Michael Borchokyo amesema.
Wataalamu wa uingereza watasaidia kukichunguza kisanduku cha kuhifadhia kumbukumbu maarufu kama Black Box.
Mtaalamu wa zamani wa masuala ya anga, David Gleave, anasema hakujawa na uhakika kisanduku hicho kitakuja na taarifa gani.
"Kama sababu ya kuanguka ni sababu hii tunayoiwaza na hasa kama mara tu ndege ilipoanguka iliharibika, basi sidhani kama kisanduku kitakuwa na kumbukumbu. Kwa kawaida kila baada ya sekunde nne hufanya kama kuzichambua taarifa ili zile za zamani zikae eneo la kuzihifadhi. Kwa hivyo tunaweza tusipate kitu chochote na ingawa kuna namna ya kurejesha kumbukumbu ya kisanduku hicho lakini tunaweza kuambulia kelele za mlipuko. Lakini kama kuharibika kwa ndege kulichukua muda kiasi basi tunaweza kuzisikia sauti za wafanyakazi wa ndege na tutaanza kufuatilia mfano mtetemo wa ndege, nguvu ya injini na mambo mengine." David Gleave, anasema.
0 comments:
Post a Comment