PAMOJA NA UJENZI WA BARABARA YA NDUNDU –SOMANGA
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe
Magufuli akipiga ngoma jana mkoani Mtwara kabla ya Ufunguzi wa Barabara
ya Masasi –Mangaka na uwekaji wa jiwe la msingi wa barabara ya Mangaka
–Mtambaswala 71.5km
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe
Magufuli wakwanza kulia akipita juu ya daraja la Nangoo Wilayani Masasi
wakati wa ukaguzi huku akifatiwa na Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi
Patrick Mfugale, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mhandis Mussa Iyombe
pamoja na Mwakilishi kutoka Benki ya Maendeleo ya Africa (ADB) Bi Tonia
Kandiero
Sehemu ya barabara ya Ndundu Somanga kama inavyooneka baada ya mkandarasi kuanza kufanya kazi kwa kasi tofauti na hapo awali
Waziri wa Ujenzi Dkt. John
Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa kijiji cha Manzese kuhusu
Mkandarasi anayejenga barabara katika eneo hilo la Ndundu Somanga kuwa
anatakiwa ndani ya miezi miwili awe amekamilisha barabara ya lami bila
visingizio vyovyote.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe
Magufuli akihutubia mbele ya viongozi mbalimbali kutoka Mkoa wa Pwani na
Wizara ya Ujenzi, ADB na wakandarasi kuhusu ujenzi wa barabara ya
Ndundu Somanga baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kufanya ukaguzi wa
maendeleo ya ujenzi wa barabar hiyo
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe
Magufuli akisalimiana na wananchi mara baada ya kuhutubia wakazi wa
Manzese katika barabara ya Ndundu Somanga mkoani Lindi
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe
Magufuli akitoa maelekezo kwa mkandarasi anayejenga barabara ya Ndundu
Somanga kuhusu kumalizia kipande cha kilometa kumi kilichobakia ndani ya
muda wa miezi miwili…Picha zote kwa Hisani ya Kitengo cha
Mawasiliano-GCU-UJENZI
………………………………………………
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe
Magufuli amempa muda wa miezi miwili mkandarasi anayejenga barabara ya
Ndundu-Somanga kufanya kazi usiku na mchana ili kumaliza kazi hiyo
haraka bila kutoa visingizio vyovyote.
Waziri wa Ujenzi aliitoa kauli hiyo juzi katika kijiji cha Manzese, Wilayani Kilwa mkoani Lindi wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika eneo hilo la ujenzi.
Aidha, Dkt. Magufuli alisema kuwa mkandarasi huyo ameshalipwa fedha zote alizokuwa ana dai hivyo anachotakiwa ni kufanya kazi kila siku usiku na mchana ili amalize kazi hiyo haraka
“Tunataka mpaka mwezi wa tisa, tuone barabara ya lami na sio vinginevyo, wahandisi wote wa mkoa wa Pwani na Lindi wamsimamie kwelikweli na kwa muda wote ili aweze kukamilisha kazi hii kwa muda tuliompa” Alisema Waziri Magufuli
Pia waziri wa Ujenzi aliwaasa Wananchi kutomwibia Mkandarasi huyo Mafuta ili aweze kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.
“Msiibe mafuta kwa mkandarasi pia nayeye anatakiwa awalipe vizuri wafanyakazi wake kwasababu sisi pia tunamlipa vizuri, pia anatakiwa atunze vifaa vyake vizuri” alisema Waziri Magufuli
Kuhusu barabara ya kutoka Lindi kuelekea Mtwara katika baadhi ya maeneo, Waziri Magufuli amewataka viongozi wa mkoa kusimamia malori yanayobeba gipsam na mawe makubwa kupita kiasi hali inayohatarisha usalama wa barabara hiyo.
“Nawataka msimamie hili pamoja na TANROADS ikiwezekana waweke mizani inayohamishika kupima malori hayo. Hii itasaidia kulinda barabara zetu ambazo tunatumia fedha nyingi kuzijenga” Alisema Dkt. Magufuli
Kuhusu udongo unaodondoka katika eneo la Mchinga, Waziri Magufuli alisema katika mwaka huu wa fedha, wizara imetenga bajeti kwa kazi hiyo ya kutengeneza eneo hilo ili tatizo lisiendele.

0 comments:
Post a Comment