Paul Scholes (kushoto) alikuwepo katika
mechi ya jumanne wakati Salford City inacheza dhidi ya Stalybridge
Celtic, klabu ambayo ana hisa, ikiwa ni mechi ya maandalizi ya kabla ya
msimu.
MANCHESTER United wamemuambia kiungo wake wa zamani Paul Scholes kuwa milango ipo wazi kwake kurudi kufanya kazi ya ukocha Old Trafford.
Scholes alikuwa sehemi ya benchi la Ryan
Giggs wakati alipokabidhiwa timu kwa muda mwishoni mwa msimu wa mwaka
jana kufuatia kufukuzwa kazi kwa kocha mkuu David Moyes.
Giggs aliingoza Man United katika mechi nne za mwisho za ligi kuu soka nchini England.
Watu walidhani Scholes ameamua kuitosa
Man United majira ya kiangazi baada ya kuwakosoa vikali baadhi ya
wachezaji wa timu hiyo kwenye fainali za kombe la dunia nchini Brazil.
Scholes aliuliza kama tayari Wayne
Roonye amepita miaka yake 28 ya ubora na aliuliza kwanini klabu
imemsajili Luke Shaw kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 30.
Inafahamika kuwa kocha wa sasa wa Man United Louis
van Gaal na mkurugenzi mkuu Ed Woodward bado wanaamini kiungo huyo
nyota wa zamani wa England ana kitu cha kuisaida klabu.
Scholes ameambiwa kuwa klabu itafurahi kama watafanya mazungumzo.
Lakini hatapewa kazi katika timu ya kwanza kutokana na Van Gaal kuridhishwa na wasaidizi wake wa sasa.
Scholes alikuwa sehemu ya benchi la ufundi la Ryan Giggs mwishoni mwa msimu wa mwaka jana.
Hata hivyo, United wanataka kumpa kazi Scholes ya kufundisha kikosi cha vijana ili asaidiane na kocha wa sasa Nicky Butt.
"Bado tunatambua thamani na ubora wa juu wa Scholes". Chanzo kutoka United kilisema.
"Milango ipo wazi kwake kurudi".
0 comments:
Post a Comment