Kodi za majengo ni chanzo kikubwa
kinachotegemewa na Halmashauri zote za Wilaya nchini zikiwemo
Halmashauri za MkoaDar es Salaam ambazo ni Ilala,Kinondoni na Temeke.
Katika kutekeleza Mpango wa
Matokeo Makubwa Sasa (BRN) hususani katika sekta ya fedha ili kuboresha
ukusanyaji wa mapato ya Serikali kupitia vyanzo mbalimbali ikiwemo kodi
ya majengo na kodi ya pango la Ardhi, mwaka 2013 Serikali iliona umuhimu
wa kodi ya majengo ndipo ikachagua vyanzo hivi kuwa mfano katika kuleta
ufanisi ili kutimiza malengo mbalimbali ya Halmashauri nchini na
kuboresha mapato ya Serikali za Mitaa.
Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya
alisema kuwa ukusanyaji wa kodi za Majengo umerudishwa kwenye Serikali
za mitaa kwa maana ndiyo wanaojua nyumba zote, ambapo hapo awali kodi za
majengo zilikuwa zikikusanywa na Mamlaka ya Mapato (TRA),na baadaye
Serikali iliona umuhimu wa Serikali za Mitaa kukusanya kodi hizi
kwasababu wao ndiyo watu ambao wapo jirani sana na wananchi na
wanafahamu nyumba zote ambazo zipo ndani ya mitaa yao.
Ili kufanikisha zoezi hili Halmashauri ziliona kuwa kuna umuhimu wa kuweka malengo ambayo yatarahisha zoezi hili.
Kwa mujibu wa taarifa ya
Utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ya Halmashauri ya
Manispaa ya Kinondoni, matangazo kwenye vyombo vya habari na vipaza
sauti ili kujenga uelewa kwa wananchi,pia kuorodhesha majengo yote
kupitia watendaji wa kata na mitaa yaliweza kutolewa na Manispaa hiyo na
kusambazwa kwenye vyombo vya habari nchini.
Waziri wa fedha, mhe. Saada Mkuya
Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Kinondoni Mwandisi Mussa Natty alisema kuwa Halmashauri yake
ina wenyeviti wa mitaa wapatao 171na watendaji wa kata 34 ambao
wanashiriki katika kufanya kazi ya kuainisha na kuorodhesha majengo kwa
uthamini.
“Tumeweza kuyafanyia uthamini
majengo 6,243 yenye thamani ya shilingi 1,493,360 na kodi inayotakiwa
kukusanywa ni shilingi 2,538,712”. Alisema Mhandisi Natty.
Mhandisi. Natty ameongeza kuwa
katika Manispaa yao wamefanya manunuzi ya vifaa vya ofisini ikiwemo
magari kumi ili kurahisisha ufuatiliaji wa mapato pia Halmashauri ya
Kinondoni imefanikiwa kuanzisha mfumo wa malipo ya kielektroniki wa
Maximalipo ambao umerahisisha malipo ya kodi katika maeneo ya karibu
zaidi,kuondoa na kupunguza msongamano wakati wa malipo,kupata kumbukumbu
za mlipa kodi kwa urahisi zaidi,uwazi na urahisi wa kufuatilia
mapungufu.
Kwa upande wa Halmashauri ya
Manispaa ya Temeke, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyoBw. Photidas Kagimbo
alisema kuwa wao wametoa mafunzo kuhusiana na uthamini kwa mkupuo kwa
maafisa watendaji wa kata 30 na wenyeviti, pamoja na watendaji wa mitaa
180 wa Manispaa hiyo.
“Tumebaini jumla ya majengo 3,860
yenye thamani ya shilingi 145,652,498 na kiasi cha kodi ni shilingi
218,478. Alisema Bw. Kagimbo.
Aidha,Bw. Kagimbo amefafanua kuwa
wamefanikiwa kuwapa watumishi uelewa wa matumizi ya TEHAMA katika
utozaji wa kodi za majengo pia halmashauri imeagiza GPS Camera 5
zitakazozosaidia kuainisha ramani za majengo katika wilaya ya TemekeMAKALA: Na Rose Masaka-MAELEZO.
0 comments:
Post a Comment