Rais Jakaya Kikwete (katikati)
akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mradi mkubwa wa Maji kwa upande wa
Wilaya ya Nachingwea katika Kijiji cha Chiumbati mkoani Lindi. Mradi huo
mkubwa wenye thamani ya Shilingi Bilioni 34.6 pia unajumlisha Wilaya ya
Masasi iliyopo Mkoa wa Mtwara. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe.
Wapili kushoto ni Waziri wa Maji, Prof Jumanne Magembe, na kushoto ni
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete. Picha na Felix Mwagara wa WMNN.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na
wananchi wa Kijiji cha Chiumbati wilayani Nachingwea baada ya kuzindua
Mradi Mkubwa wa Maji kwa upande wa Wilaya ya Nachingwea, Mkoa wa Lindi.
Mradi huo mkubwa wenye thamani ya Shilingi Bilioni 34.6 pia unajumlisha
Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara. Kushoto aliyekaa ni Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias
Chikawe akifuatiwa na Waziri wa Maji, Prof Jumanne Magembe. Picha na
Felix Mwagara wa WMNN.
Rais Jakaya Kikwete akimtwisha
ndoo ya maji Mkazi wa Nachingwea mjini mara baada ya kuzindua mradi
mkubwa wa maji wenye thamani ya Shilingi Bilioni 34.6 unaojumlisha
Wilaya ya Nachingwea na Masasi mkoani Mtwara. Kulia ni Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias
Chikawe akifuatiwa na Waziri wa Maji, Prof Jumanne Magembe. Picha na
Felix Mwagara WMNN.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akimshukuru
Rais Jakaya Kikwete kwa kuzindua Mradi Mkubwa wa Maji jimboni kwake
Nachingwea mkoani Lindi. Mradi huo wa Maji wenye thamani ya Shilingi
Bilioni 34.6 unajumlisha Wilaya ya Nachingwea na Masasi iliyopo Mkoa wa
Mtwara. Katika hotuba yake fupi ya kumshukuru Rais Kikwete, Waziri
Chikawe alisema jimbo lake lilikuwa linateseka na shida ya maji kwa
kipindi kirefu lakini sasa tatizo hilo limekwisha. Picha zote na Felix
Mwagara wa WMNN.
0 comments:
Post a Comment