Iman Kajula Ofisa Mtendaji Mkuu wa
kampuni ya EAG Group akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi
wa Idara ya Habari Maelezo leo mchana kuhusu maonyesho ya NANE NANE
yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mkoani Lindi, Kutoka kulia ni Mathew
Gugae Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Biashara EAG Group na katikati
ni Engerbelt Moyo Mwenyekiti wa TASO.
WANANCHI mkoani Lindi wanatarajiwa
kuelimishwa njia bora na za kisasa za uvuvi, ufugaji na ukulima ili
waweze kuboresha kipato chao na Taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dar
es Salaam na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wakulima Tanzania(TASO) Engelbert
Moyo wakati akiongea na waandishi wa habari.
Amesema kuwa wakati wa maonesho ya
nanenane ambayo Kitaifa yanafanyika mkoani Lindi watajitahidi
kuhakikisha wananchi wanajifunza teknolojia mpya za kilimo, ufugaji na
uvuvi ili waweze kuzalisha mazao yanayokidhi viwango vya Kitaifa na
Kimataifa.
Moyo ameongeza kuwa watawaelimu wavuvi juu ya madhara ya uvuvi haramu na unavyohatarisha mazingira na viumbe wa majini.
Aidha Mwenyekiti huyo amesema kuwa
maonesho yatafunguliwa na Rais wa Serikali za Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein na kufungwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete.
Amesema kuwa Mawaziri mbalimbali
watasaidia kutoa elimu kwa wakazi wa Mkoa huo kuhusu shughuli mbalimbali
wanazozifanya katika kuwaletea maendeleo.
Na Rose Masaka -MAELEZO
0 comments:
Post a Comment