Wednesday, 23 July 2014

YANGA SC KUFUNGUA DIMBA RAYON KAGAME AGOSTI 8

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM

YANGA SC itafungua dimba na wenyeji Rayon Sport Uwanja wa Amahoro, Kigali nchini Rwanda katika Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame Agosti 8, mwaka huu.
Katika ratiba ya michuano hiyo iliyopangwa leo mjini Kigali, KMKM ya Zanzibar ambayo ipo kundi moja A na Yanga, itafungua pazia la michuano hiyo mchana wa siku hiyo kwa kumenyana na Atlabara ya Sudan Kusini. 
Yanga itaanza na Rayon Kombe la Kagame

Yanga SC itarudi tena dimbani, Agosti 10 kumenyana na jirani zao KMKM, kabla ya kucheza na Atlabara Agosti 12 na kukamilisha mechi za kundi lake, kwa kumenyana na Coffee ya Ethiopia Agosti 16.
Wawakilishi wa Tanzania, Yangs SC wanatarajiwa kuingia kambini Agosti 1, mwaka huu kisiwani Pemba kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo ya 40. Yanga SC inayofundishwa Marcio Maximo anayesaidiwa Leonardo Neiva, wote Wabrazil na mzalendo Salvatoty Edward, imetwaa mara tano taji la michuano hiyo, 1975 visiwani Zanzibar, 1993 na 1999 mjini Kampala, Uganda na mara mbili mfululizo pia 2011 na 2012 mjini Dar es Salaam. Maana yake watakwenda Kigali mwezi ujao kujaribu kusawazisha rekodi ya wapinzani wao wa jadi, Simba SC waliotwaa mara sita, 1974, 1991 mjini Dar es Salaam, 1992 visiwani Zanzibar, 1995, 1996 mjiji Dar es Salaam na 2002 Zanzibar tena. Rais Paul Kagame wa Rwanda ndiye mlezi wa mashindano haya ambaye hutoa dola za Kimarekani 60,000 kila mwaka kwa ajili ya zawadi. Wizara ya Michezo ya Rwanda na mashirika mengine yatadhamini michuano hiyo, itakayokwenda sambamba na maazimisho ya miaka 20 ya mauwaji ya kimbau. Televisheni ya kulipia ya Supersport ya Afrika Kusini ambao ni maswahiba wa muda mrefu wa CECAFA, ni miongoni mwa wadhamini pia na wataonyesha mechi zote za michuano hiyo moja kwa moja. 
Mtihani wa kwanza wa Maximo na Jaja ni Kombe la Kagame

RATIBA KAMILI KOMBE LA KAGAME 2014

KUNDI A: 
Rayon Sport (Rwanda)
Yanga SC (Tanzania)
Coffee (Ethiopia)
KMKM (Zanzibar)
Atlabar (Sudan Kusini)
KUNDI B
APR (Rwanda)
KCC (Uganda)
Fambeau de L’Est (Burundi)
Telecom (Djibouti)
Gor Mahia (Kenya)
KUNDI C:
Vital’O (Burundi)
El Merreikh (Sudan)
Polisi (Rwanda)
Benadir (Somalia)
RATIBA KOMBE LA KAGAME 2014:
Agosti 8, 2014:
Atlabara Vs KMKM A NYAMIRAMBO
Rayon Vs Yanga A AMAHORO
Gor Mahia Vs KCCA B AMAHORO
Agosti 9, 2014:
Vital ‘O’ Vs Banadir C AMAHORO
Police Vs El Mereikh C AMAHORO
APR Vs Flambeau B AMAHORO
Agosti 10, 2014:
KMKM Vs Young A AMAHORO
Telecom Vs KCCA B NYAMIRAMBO
Coffee Vs Rayon A AMAHORO
Agosti 11, 2014:
Banadir Vs El Mareikh C NYAMIRAMBO

Gor Mahia Vs Flambeau B NYAMIRAMBO
Vital’O Vs Police C NYAMIRAMBO
Agosti 12, 2014: 
KMKM Vs Coffee A NYAMIRAMBO
Yanga Vs Atlabara A NYAMIRAMBO
Agosti 13, 2014: 
APR  Vs Telecom B NYAMIRAMBO
KCCAVs Flambeau B NYAMIRAMBO
Agosti 14, 2014: 
Coffee Vs Atlabara A NYAMIRAMBO
Rayon  Vs KMKM A NYAMIRAMBO
Police Vs Banadir C NYAMIRAMBO
Agosti 15, 2014:
Flambeau Vs Telecom B NYAMIRAMBO
APR Vs Gor mahia B NYAMIRAMBO
El Mareikh Vs Vital’O C NYAMIRAMBO
Agosti 16, 2014:
Coffee Vs Yanga A NYAMIRAMBO
Rayon Vs Atlabara A NYAMIRAMBO
Agosti 17, 2014: 
Telecom Vs Gormahia B NYAMIRAMBO
KCC Vs APR B NYAMIRAMBO
Agosti 18, 2014 (MAPUMZIKO)
Agosti 19, 2014:
ROBO FAINALI- NYAMIRAMBO
Agosti 21, 2014 (MAPUMZIKO)
Agosti 22, 2014:
NUSU FAINALI- AMAHORO
Agosti 23, 2014 (MAPUMZIKO)
Agosti 24, 2014:
MSHINDI WA TATU- AMAHORO
FAINALI-  AMAHORO
(Michuano itaonyeshwa moja kwa moja na Televisheni ya SuperSport ya Afrika Kusini)

0 comments: