Imechapishwa Julai 26, 2014, saa 6:53 mchana
Aliyewahi kuwa Kocha Msaidizi wa Taifa Stars,
Sylvester Marsh, amesema uwezo ulioonyeshwa na timu hiyo katika mechi yake
dhidi ya Msumbiji ni mkubwa na anaamini itashinda katika mchezo wa marudiano.
Stars ilikutana na Mambas ya
Msumbiji wiki iliyopita katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la
Mataifa ya Afrika inayotarajiwa kufanyika mwakani nchini Morocco ambapo katika
mchezo wa awali, ilifanikiwa kutoka sare ya mabao 2-2.
Mambas ni moja kati ya timu ambazo zimekuwa
zikiisumbua Stars kwa muda mrefu pindi zinapokutana nayo.
Marsh amesema kuwa mwenendo wa timu hiyo kwa sasa
ni mzuri kufuatia maandalizi waliyoyafanywa na kuwataka Watanzania wasiwe na
haraka ya kupata mafanikio, kwani hali hiyo hutokea hata katika maisha ya
kawaida.
“Uwezo wa Stars kwa sasa upo juu ya Mambas kwa
jinsi nilivyowaona walivyocheza katika mechi ya kwanza licha ya kutoka sare,
hivyo nina imani kubwa kuwa itashinda na kuitoa katika mchezo wa marudiano.
“Tumeweza kuona katika mchezo wa awali
tulifanikiwa kuitoa Zimbabwe licha ya kuwa na matokeo mabaya ya awali katika
uwanja wa nyumbani.
“TFF imejitahidi kwa kiasi kukubwa kuiandaa timu
hiyo kwa kukaa kambi kwa muda mrefu na kuipeleka nje ya nchi kwa ajili ya
kujiandaa pamoja na kucheza mechi za kirafiki, ambapo imebadilika kwa kiasi
kikubwa, hivyo ni vyema wadau wakawa na subira kuhusiana na suala hilo ili timu
iweze kufanya vizuri hapo baadaye,” alisema Marsh.
Chanzo: Salleh Ally
0 comments:
Post a Comment