Monaco na Atletico Madrid wanaitaka saini ya Fernando Torres.
Imechapishwa Julai 23, 2014, saa 6:00 asubuhi
KLABU ya Monaco imeingia katika vita na Atletico Madrid kuiwinda saini ya mshambuliaji wa Chelsea, Fernando Torres.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania
mwenye miaka 30 anahitaji kutafuta timu ya kupata nafasi ya kucheza,
lakini Chelsea watasikiliza ofa nzuri zaidi.
Bluu ya kweli: Torres anaweza kugoma kuondoka Chelsea baada ya kuwasili kwa Cesc Fabregas
Atletico Madrid wanavutiwa kumrudisha nahodha huyo wa zamani wa Vicente Calderon baada ya kumuuza nyota wake Diego Costa katika klabu ya sasa ya Torres ya Chelsea.
Chelsea wapo tayari kumuuza Torres kama ofa ya paundi milioni 20 itapatikana.
Msimu ujao, Jose Mourinho anataka kumtumia mshambuliaji mmoja tu ambapo Diego Costa ndiye atakuwa mshambuliaji namba moja.
Nafasi ya Torres itafifia zaidi kama Didier Drogba atarudi London Magharibi.
Jembe jipya: Diego Costa atabadili nafasi ya Torres
0 comments:
Post a Comment