HOME »
» TFF YA FUNGA SEMINA KWA MAREFA WA TANZANIA
RAIS
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema kwamba
sekta ya marefa nchini inatia aibu kwa sababu ipo chini mno na amewataka
viongozi wa sekta hiyo kuhakikisha wanaiinua juu.
Akizungumza
leo wakati wa kufunga semina ya marefa wa Shirikisho la Soka la
Kimataifa (FIFA) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Malinzi amesema
kwamba ipo haja ya jitihada kubwa kufanyika kuinua sekta hiyo.
Malinzi
amesema baadhi ya nchi jirani ikiwemo Kenya zilikuwa na marefa katika
Kombe la Dunia mwaka huu nchini Brazil, lakini Tanzania haikuwa na refa
hata mmoja.
Amesema
hata kwenye michuano mingine ya barani, kama Kombe la Mataifa ya Afrika
(AFCON) bado ushiriki wa marefa wa Tanzania ni duni.
|
Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) akimkabidhi cheti cha kuhitimu semina ya marefa, Israel Mujuni Nkongo kulia |
|
Malinzi akiwahutubia marefa pembeni ya mkufunzi wa FIFA, Carlos Henriques kutoka Afrika Kusini |
|
Katika picha ya pamoja na Malinzi na wahitimu baada ya semina hiyo |
Malinzi
ameshauri vyuo vya elimu ya juu nchini navyo visaidie kutoa mafunzo ya
urefa, akitolea mfano Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambao wana
somo la Elimu ya Viungo inayohusu mwili wa mwanamichezo (PE).
“Mfano
pale UD (Chuo Kikuu Dar es Salaam) wana somo la PE, kama wataamua kutoa
mafunzo ya urefa sisi (TFF) tutakuwa tayari kuwapa ushirikiano ili
kuhakikisha tunainua viwango vya marefa nchini,”amesema Malinzi.
Malinzi
amesema kwamba amesikitishwa na mkoa wa Ruvuma alipoutembela hivi
karibuni na kukuta una marefa wanane tu, wakati ni mkubwa na una wilaya
nyingi.
“Nilishangaa
sana, mkoa mkubwa kama ule una marefa wanane tu, sasa huyo bingwa wa
mkoa anapatikana vipi, kwa kweli hali ni mbaya sana,”amesema.
Malinzi
amesema baada ya hali hiyo, ameagiza TFF ifanye tathmini ya kujua kila
mkoa una marefa wangapi ili kujua sehemu ambazo wana mapungufu waelekeze
nguvu ya kuinua marefa.
Amesema
ipo haja ya waamuzi wastaafu, wakongwe na viongozi wa marefa
kushirikiana kuinua marefa chipukizi katika viwango vizuri ili taifa
liwe na marefa wa kutosha siku za usoni.
Pamoja
na hayo, Malinzi amewaasa marefa kujiepusha na rushwa- kwani soka ya
Tanzania kwa sasa inanyemelewa na maharamia wa kimataifa wa kupanga
matokeo ili kujinufaisha katika mchezo wa kamari.
“Nina
ushahidi wa kutosha mechi za Tanzania sasa zinachezewa kamari nje ya
nchi, sasa hii ni hatari sana kwa soka yetu, naomba sana mjiepushe na
upangaji wa matokeo,”amesema.
Malinzi
amesema TFF inawafanyia uchunguzi marefa wawili kwa tuhuma za kupanga
matokeo ambao kwa sasa wamesimamishwa ili kupisha uchunguzi huo, na
ikibainika ni kweli watachukuliwa hatua kali za kisheria.
“Nchi
za wenzetu ukigundulika ulihusika na upangaji wa matokeo, unapelekwa
mahakamani sheria inafuata mkondo wake, sasa na sisi tutafanya nini, kwa
hiyo naomba sana tujiepushe na upangaji wa matokeo,”Malinzi aliwaambia
marefa huyo.
Semina
hiyo iliendeshwa na mkufunzi wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA),
Carlos Henriuques kutoka Afrika Kusini ambaye ni Ofisa Maendeleo ya
Marefa wa shirikisho hilo.
0 comments:
Post a Comment